MKOA wa Geita unaongoza kuwa na wanaume wenye wapenzi zaidi ya
mmoja ukifuatiwa na mikoa ya Lindi, Dar es Salaam, Iringa na Mtwara.
Takwimu hizo zilitangazwa jana na Mkurungenzi Mkuu wa Tume ya Kuzuia na Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), Fatma Mrisho wakati wa uzinduzi wa takwimu za viashiria vya maambukizi ya virusi vya ukimwi na malaria.
Alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2011/2012, kwa sasa hali ya maambukizi imepungua ambapo idadi ya watu na maambukizi ni asilimia 5.1 kutoka 5.8 ya mwaka 2008.
Mrisho alibainisha kuwa kiwango cha maambukizi ya ukimwi kimkoa kwa sasa ni Njombe asilimia 14, Iringa (9.1), Mbeya (9), Mara (7.5) Ruvuma (7), Dar es Salaam (6.9), Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9), Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita asilimia 4.7.
Mikoa mingine ni Mwanza asilimia 4.2, Mtwara (4), Morogoro (3.8), Kilimanjaro (3.8), Simiyu (3.6), Kigoma (3.4), Singida (3.3), Arusha (3.2), Dodoma (2.9), Tanga (2.4), Manyara (1.5), (Unguja (1.2) na Pemba asilimia 0.3.
Mrisho aliitaja mikoa inayoongoza kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja, yaani mwanaume mmoja kutembea na zaidi ya wanawake watano ni Geita asilimia 32, Lindi (30), Dar es Salaam (29), Iringa (27) na Mtwara asilimia 22.
Hatua hiyo ilikemewa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake, akiwaomba wanaume kuwa chanzo cha mabadiliko ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Mikoa inayoongoza kuwa na wanaume wasiotahiriwa ni Njombe asilimia (49), Katavi (44), Kagera (39), Mbeya (38), Rukwa (28) na Simiyu asilimia 30.

No comments :
Post a Comment