Top News
Showing posts with label Lady JayDee. Show all posts
Showing posts with label Lady JayDee. Show all posts

Monday, September 16, 2013

Lady Jay Dee Afunguka Kilicho mkuta hadi kuanguka jukwaani...

 

 
 
Lady Jaydee akiwa backstage na kiatu chake kilichosabisha ateleze jukwaani
Katika show hiyo Lady Jaydee alinunua kiatu cha rangi ya blue, kirefu aka high heels chenye thamani ya shilingi 168,000. Yes laki moja na elfu sitini na nane kama masikio yetu hayakutudanganya.
Hata hivyo urefu wa kiatu hicho ameutaja kuwa chanzo cha kuteleteza jukwaani kwenye show hiyo na kukaribia kumwangusha.
“Kuanguka jukwaani ni ajali kama ajali zingine, isitoshe sikuanguka bali nilikaribia. Ila poleni kwa mlioumizwa na hicho kitendo…Nitapunguza urefu wa viatu siku nyingine,” aliandika jana kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Ni bahati mbaya tu, kwani hata Mwanza/Kahama/Dodoma vilikuwa virefu kama hivyo hivyo na sikuteguka,” alitweet kufafanua kuhusu uvaaji wa viatu virefu jukwaani
Read more ...

Thursday, August 1, 2013

Nyota ya Lady Jaydee Yazidi kung'ara Si Joto Hasira sasa ni Yahaya.


Lady Jaydee na wimbo wake Yahaya ameendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye Marimba Music Charts,MMC, kwa wiki ya pili mfululizo.

Ngoma ya Madee, Sio Mimi imeendelea kufanya vizuri kwa kupanda kwa nafasi moja hadi nafasi ya 2 kutoka nafasi ya tatu wiki iliyopita. Majanga ya Snura imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 5 wiki iliyopita hadi nafasi ya 5 wiki hii.


Wiki hii Bila Kukunja Goti ya Mwana FA na AY waliyomshirikisha J.Martins imeingia kwa kishindo kwenye MMC hadi nafasi ya 6 wiki hii huku My Baby wa Quick Rocka ikiingia kwa mara ya kwanza hadi nafasi ya 9.


Marimba Music Charts huandaliwa kila wiki kutokana na chart za radio zote nchini.
Read more ...

Tuesday, July 16, 2013

Lady JayDee Aamua kumuweka Yahaya hadharani Aachia picha mtandaoni.

Mwigizaji maarufu wa filamu hapa Bongo, Kulwa Kikumba maarufu zaidi kama Dude, amechukua shavu la kucheza kama Yahaya katika video ya hitsong ya lady jay Dee ambayo upigaji picha zake unatarajiwa kukamilika leo.

Ogopa Videos kutoka Kenya ndio wakali ambao wanasimamia mchongo mzima na kufanya mitaa yote hivi sasa kusubiria kwa hamu kuona kazi hii itakapokamilika itakuwaje hasa kutokana na umahiri wa Dude katika kuigiza.


Read more ...
Designed By ApexbnewZ