Top News
Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Friday, October 18, 2013

CHADEMA wamwaga nyaraka za 'siri' Hesabu za Ruzuku; Msajili na CAG wawajibike

C/HQ/ADM/KUH/18 17/10/2013


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI JUU YA AGIZO LA KAMATI YA BUNGE (PAC) KUHUSU VYAMA KUTOKUKAGULIWA NA CAG TANGU MWAKA 2009-2013.
Kutokana na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuwa vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi cha miaka minne mfululizo, yaani kuanzia mwaka 2009/2010- 2012/2013.

CHADEMA tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo juu ya taarifa hizo;

i. Kuwa taarifa hizo sio sahihi na hazina ukweli kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine, hii ni kutokana na ukweli kuwa tulishawasilisha taarifa zetu za fedha kwa msajili wa vyama vya siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011, 2011/2012 na hili linathibitishwa na barua ya msajili wa vyama vya siasa yenye Kumb.Na. CDA.112/123/01a/37, ya tarehe 04 september 2012. Iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa (nakala imeambatanishwa).

Aidha, hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/2010, tuliziwasilisha kwa Msajili wa vyama vya siasa kwa barua yenye Kumb.Na. C/HQ/ADM/MSJ/04/71 ya tarehe 27 Octoba, 2011. (Nakala ya barua imeambatanishwa).

ii. Kuhusu taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa mwaka huu wa fedha 2012/2013, bado haijawasilishwa kwenye ofisi za msajili wa vyama kutokana na barua ya msajili wa vyama vya siasa ya Novemba 26, 2012 yenye Kumb.Na.DA.112/123/16A/97 ambayo ilikuwa na maelekezo kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa, iliyokuwa inajibu barua tuliyomwandikia tukitaka kupata ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa hesabu za chama kutakiwa kufanywa na CAG na alitujibu kuwa “tumefanya mawasiliano na Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali (CAG) kwa ufafanuzi wa jambo hili na tutawafahamisha ipasavyo kuhusu malipo/gharama mliyotakiwa kulipa katika ukaguzi wa Mahesabu hayo”; mpaka leo hatujawahi kupata ufafanuzi huo pamoja na ukweli kuwa tumeshafunga hesabu zetu za mwaka kama chama (barua imeambatanishwa).
iii. Kuhusu taarifa ya fedha kutoka nje ya nchi, CHADEMA tumekuwa tukiwasilisha taarifa zetu kila mara tunapopata fedha kwa ajili ya mafunzo na programu nyingine mbalimbali za chama kama ambavyo msajili alituandikia barua tarehe 19 Agosti 2013 yenye Kumb. Na.DA.112/123/16a/10 iliyokuwa ni taarifa ya mapato yatokanayo na michango au misaada toka nje ya nchi, alisema “tunashukuru kwa taarifa hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya vyama vya siasa” (imeambatanishwa barua husika).

iv. Kuhusu Taarifa za gharama za uchaguzi kwa mwaka 2010 , tuliwasilisha taarifa hiyo na Msajili alikiri kuwa ni vyama viwili tu ndiyo vilikidhi utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi kwa ukaguzi wa marejesho, hii inathibitishwa na barua ya Msajili yenye Kumb.Na. CDB.173/205/01/23 ya tarehe 16 April, 2012. (Nakala imeambatanishwa).

Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa CHADEMA ndiyo ambayo tulidai CAG awe na mamlaka ya kukagua fedha za vyama vya siasa ili taarifa zake ziwekwe hadharani na tutaendelea kutoa ushirikiano kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote, kuhakikisha sheria hii inatekelezwa ipasavyo kuhakikisha uwazi kwenye mapato na matumizi ya vyama vya siasa.

Aidha, kama ambavyo siku zote tumesimamia na kusisitiza, tunamtaka CAG akague fedha zote za vyama na sio ruzuku tu kama ambavyo kamati ya Bunge inataka iwe.


Imetolewa leo Alhamis, Oktoba 17, 2013;

……………………….
Antony C. Komu
Katibu wa Baraza la Wadhamini. 





Read more ...

Thursday, October 10, 2013

Zitto Kabwe Ataja Mshahara anaolipwa waziri mkuu kwa Mwezi

HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameweka wazi mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Zitto ameutaja mshahara huo wa Pinda anayejitambulisha kama ‘mtoto wa mkulima’ juzi mjini Mpanda na jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama.

Alisema Pinda anapokea jumla ya sh milioni 26, ambazo ni kiasi kikubwa kulinganisha na uchumi wa nchi.

Akichanganua alisema Pinda anapokea sh mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya waziri na kiasi kinachosalia kufikia sh mil. 26 kwa nafasi yake ya uwaziri mkuu.

Alisema sababu hiyo ya mishahara mikubwa isiyokatwa kodi ndiyo huwafanya viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakali pale vyombo vya habari vinapotaka kuwafahamisha wananchi namna watumishi wao wanavyojilipa.

“Nimeanza na mshahara wa waziri mkuu pia siku zijazo nitataja na wa rais, kwa kuwa amesaini makubaliano na Serikali ya Marekani kuendesha nchi kwa uwazi, na moja ya uwazi ni kwa muajiri kujua kiasi anachomlipa mwajiriwa wake,” alisema Zitto.

Hatua ya Zitto imekuja baada ya kuwapo mvutano mkubwa kuhusiana na kile kinachodaiwa ‘usiri’ wa mishahara ya watumishi wa umma, wakati ni haki ya walipa kodi kujua kile wanachowalipa walioomba kuwaongoza.

Kodi ya laini za simu

Akizungumzia sakata la kodi katika laini za simu, Zitto alisema CCM ina ajenda ya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Alisema serikali baada ya kubaini watu wengi wanapeana taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi, hususan katika masuala ya kisiasa, wakaona njia sahihi ya kudhibiti ni kuwatoza kodi ya laini ili kupunguza hatari ya mawasiliano hayo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

“Sikuwepo bungeni wakati wabunge wa CCM wanapitisha kadhia hiyo ya kuwanyonya wananchi, wenzangu wakaniambai tukasema hapana, kwa maana tuliona hii leo kuna Watanzania wengi wasio na uwezo wa kuhudumia simu kwa kiasi cha sh 1,000 kwa mwezi,” alisema Zitto.

Akijibu maswali ya wananchi mjini Mpanda waliotaka kujua sababu ya kupunguza makali bungeni, Zitto alisema hakuna makali yaliyopungua bali ni mitazamo ya watu.

Alisema kwa kushirikiana na wabunge wenzake wa upinzani wamekuwa wakisimamia hoja zenye manufaa kwa wananachi huku wabunge wanaojipambanua kuwa majasiri kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwaunga mkono wazi wazi.

Akiwa  wilayani Sikonge, Zitto alisema Watanzania hawawezi kujivunia uhuru huku mama zao, watoto wao na wazee wao wakiwa hawana uhakika wa kupata huduma bora ya afya, elimu na maji safi.

Alisema kwa sasa Tanzania ni taifa moja lililogawanyika katika nchi mbili za wenye fedha na wasio na fedha.


Alisema nchi ya wenye fedha, familia zao husoma katika shule bora, zenye mazingira bora na walimu wazuri, hutibiwa katika hospitali zenye hadhi na huduma muhimu na ikibidi nje ya nchi, huku nchi ya wasio na fedha  familia zao wakiishi kwa shida, kusoma katika majengo ya shule na walimu wasiopata mishahara ya kuridhisha na hospitali zisizokuwa na huduma muhimu licha ya kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya bima ya afya.
Source:Tanzania Daima
Read more ...

Wednesday, October 2, 2013

Hizi ndio sababu za msingi zilizo sababisha Mh Lema Kufutiwa Kesi iliyokua inamkabili!




MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), jana alitikisa Jiji la Arusha baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumfutia kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili.

Lema alidaiwa kutoa kauli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alienda kwenye Chuo cha Uhasibu Arusha kama anaenda kwenye sherehe za kuaga mtoto wa kike “send off”.


Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Devota Msofe baada ya wakili wa serikali, Eliananyi Njiro, kutumia kifungu cha 20 kifungu kidogo cha 1 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kuliondoa shauri hilo ambalo lilikuwa lianze kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo. Upande wa serikali ulipanga kuleta mashahidi tisa.


Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliofurika mahakamani hapo kusikiliza mwenendo wa kesi hiyo waliupokea uamuzi huo
kwa shangwe kubwa.


Akizungumza nje ya mahakama mara baada ya uamuzi huo, Lema alisema kuwa alikuwa anajua shauri hilo ni la kutengenezwa ndiyo maana mashahidi wengi walikuwa ni polisi.


“Ni kama nimeshinda kesi, na Mungu ameendelea kutupigania, na tutaendelea kupambana kutafuta haki bila hofu maana miili yetu na nafsi zetu zimeishapoteza maumivu kwa sababu ya mateso yaliyojaa uongo na hila.


“Tutaendelea na kelele zetu za kupigania haki bila kurudi nyuma huku uvumilivu ukiwa nguzo yetu kubwa,” alisema Lema.

Hata hivyo, alikiri kutamka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mulongo alienda Chuo cha Uhasibu kama anaeenda kwenye “send-off” kwani yeye ndiye alimpigia simu akimtaka afike kusikiliza kero za wanachuo, lakini hakulipa uzito unaostahili suala hilo hasa ikizingatiwa kuwa pale kuna mwanachuo alikuwa amepoteza maisha.

Lema alisema kuwa wanaweza kuwa wamemfutia kesi hiyo ili kesho wamfungulie nyingine jambo alilodai kuwa yuko tayari kwani anaelewa kuwa lengo ni kutaka kumuogopesha ili aache kuwatetea wananchi kitu alichodai kuwa hawatafanikiwa kwani tayari ana ganzi mwilini mwake, hivyo haogopi kufa, kesi wala kufungwa.


Kwa upande wake wakili wa Lema, Method Kimomogoro alisema kuwa ni vema kama serikali ingeamua kutumia busara ya kuona hakuna kesi toka awali, hivyo wasingefungua kabisa shauri hilo lililopoteza muda wa
mahakama na mteja wake, kwani hata maelezo ya kesi yalionyesha dhahiri hakukuwa na kosa la uchochezi.


Alisema kuwa sheria inaruhusu kumfurahia, kumkejeli au kumzomea mtu, ndiyo maana hata bungeni wanaonekana waheshimiwa wakizomeana na kurushiana vijembe, na akadai hata kauli iliyodaiwa kutolewa na Lema dhidi ya mkuu wa mkoa ilikuwa kijembe tu.


Kimomogoro alilitaka Jeshi la Polisi kutenda kazi zao kwa mujibu wa sheria, huku akiwataka warudi kwenye hoja ya msingi na wawaeleze wananchi endapo wameshawakamata waliohusika na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mnamo Aprili 24, mwaka huu, mshtakiwa Lema akiwa eneo la Freedom Square ndani ya Chuo cha Uhasibu, alitoa maneno ya uchochezi yaliyosababisha uvunjifu wa amani.


Maneno hayo yanayodaiwa kutamkwa ni kinyume na kifungu cha 390 sura ya 35 cha sheria ya kanuni ya adhabu, marejeo ya mwaka 2002 .


“RC anakuja (Chuo cha Uhasibu) kama anaenda kwenye send-off, hajui chuo kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hicho... (RC) Ameshindwa hata kuwapa (wanafunzi) pole kwa kufiwa na amesema hawezi kuongea na
wanafunzi wasio na nidhamu.” Yalinukuliwa baadhi ya maneno yaliyodaiwa kuwa yalitamkwa na Lema.


Kauli hizo zinadaiwa zilipandisha hasira za wanafunzi ambao walianza kumrushia mawe na chupa Mkuu wa Mkoa, Mulongo alipokuwa akiwahutubia kuhusiana na tukio la kifo cha mwanafunzi, Henry Koga kilichotokea Aprili 23, mwaka huu.

Read more ...

Tuesday, October 1, 2013

CUF, CHADEMA na NCCR Mageuzi waendelea kutangaza hali ya hatari tarehe 10 Mwezi huu.




MUUNGANO wa vyama vitatu vya upinzani umesema kuanzia sasa haupo tayari
kubatilisha kusudio lao la kufanya maandamano nchi nzima kwa kukutana na
kiongozi yeyote isipokuwa tu Rais Jakaya Kikwete atapotangaza kutosaini
muswada uliopitishwa bungeni kinyemela. Pia umesema hautakubali kamwe
kuzuiwa na chombo chochote kufanya maandamano na mikutano ifikapo Oktoba
10 mwaka huu.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Viongozi wa Kamati ya Ufundi ya
Muungano wa vyama vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.

Hao ni Mkurugenzi wa
Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, Mkuu wa Idara na Taasisi za
Dola na Vyombo vya Uwakilishi NCCR Mageuzi, Faustine Sungura na Naibu
Mkurugenzi wa Habari na Haki za Binadamu na Uhusiano wa Umma kutoka CUF,
Abdul Kambaya.

Mnyika alisema uamuzi huo umefikiwa kwa pamoja
na wenyeviti wa vyama hivyo vitatu kwamba muda uliobaki sasa hadi
kufikia Oktoba 10 mwaka huu ni wa kukutana na makundi maalumu kuwaeleza
kasoro zilizopo kwenye mswada na kuwashawishi kuwaunga mkono.

“Tunapenda
kuwaeleza vyama vitatu tayari vimekamilisha maandalizi ya kufanya
mikutano nchi nzima, tumejipanga kupinga Rais Kikwete kusaini muswada
huo kwa njia mbalimbali zikiwamo za demekrasia, maandamano na raia.

“Jambo
hili ni kubwa na lina maslahi kwa kila Mtanzania, hivyo tunaomba kila
kundi na taasisi ziungana na sisi na kufanya maandamano kwa njia ile
watakayoona inafaa na hata kufanya mgomo.

“Viongozi wa dini
wanaweza kuandaa sala ya kuliombea taifa kupinga Rais Kikwete kutosaini
muswada huo, hivyo hivyo katika taasisi nyingine kulingana na nafasi
zao, nasema siku hiyo itakuwa ni ya kupinga kila kitu.

Kama
ikitokea kundi linazuia mikutano hiyo au maandamano hayo kwa kusema tii
sheria bila shuruti, kamwe mtu asikubali kuzuiwa, yaani tunataka siku
hiyo iwe ya kupinga kila jambo litakalijitokeza kwa lengo la
kukwamisha,alisema.

Abdul Kambaya kutoka CUF, alisisitiza
kumuomba Rais Kikwete kutosaini muswada huo na badala yake kuurudisha
bungeni kuufanyia marekebisho ambayo yanalalamikiwa

-Mtanzania
Read more ...

Thursday, September 19, 2013

Maandamano ya CHADEMA, CUF na NCCR yapigwa marufuku siku ya jumamosi

Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya umoja wa vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA siku ya Jumamosi yaliyokuwa yamepangwa  kuanzia Tazara hadi Jangwani na Mwenge hadi Jangwani na sehemu mbalimbali ...

Taarifa  iliyotolewa  na kamanda Kova  kupitia  ITV   imeeleza  kuwa  Polisi wamechunguza na kugundua kwamba  maandamano  hayo  yataleta usumbufu kwa watu wengine na kwamba kwa kuwa lengo ni kufika Jangwani basi Viongozi wa vyama hivyo wawaambie wafuasi wao waende Jangwani bila Maandamano.

Source: ITV

Read more ...

Lowasa adondosha ujumbe mzito kwa wasio mpenda Usome hapa.

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema yuko imara na hakatishwi tamaa na maneno ya baadhi ya wanasiasa dhidi ya harakati zake za kisiasa.
Lowassa ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati akizungumza katika harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la African Inland Church of Tanzania (AICT) mjini Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Alisema, wanasiasa wanaomshambulia na kueneza mabaya dhidi yake hawambabaishi.
“Si nia yangu kuwajibu hao wanaonisema sema..mimi niko imara kama ilivyo kuwa jana, juzi..na nitaendelea kuwa imara kwani naamini anayenilinda bado yuko na mimi. Nayaweza haya yote kwa yeye anitiaye nguvu,” alisema Lowassa.
Lowassa alirejea kauli yake ambayo alikwishaitoa hadharani mara kadhaa, kuwa yeye siyo tajiri wa fedha bali wa watu na kuwashangaa wale ambao wamekuwa wakihangaika kuwajua marafiki zake wanaomsindikiza katika harambee za kuchangia shughuli za kimaendeleo anazozifanya katika sehemu mbalimbali nchini.
Kabla ya Lowassa kuzungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, alisema kuwa kuna kikundi cha wanasiasa wahuni wanaojaribu kumkatisha tamaa Lowassa kwa maneno machafu dhidi yake.
“Kuna kikundi cha wanasiasa wahuni, wenye wivu na roho ya korosho dhidi ya Lowassa, wanasema sema maneno ya hovyo hovyo ya kihuni, lakini sisi tunasema usikate tamaa huo ni wivu tu, kazi unazozifanya kulitumikia taifa hili kila mtu anaziona,” alisema Mgeja.
Kauli hiyo ya Mgeja inafuatia kauli zenye mwelekeo wa shutuma ambazo amekuwa akielekezewa Lowassa na baadhi ya wanasiasa, kuwa anatumia fedha chafu kuchangia shughuli za maendeleo ya kijamii.
-Mtanzania
Read more ...

Hii ndio maana ya "PEOPLES POWER" ya CHADEMA kwa mujibu wa Waziri MAGUFULI soma hapa Alivyo itafsiri.

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amesema kuwa anafurahishwa na salamu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kuwa kila neno katika salamu hiyo lina maana na linaashiria ushindi.
Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa sekta ya miundombinu ya barabara wa Mkoa wa Iringa, katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Christine Ishengoma.
Alisema neno ‘People’ linamaanisha Watanzania waliompigia kura Rais Jakaya Kikwete na ‘Power’ likiwa na maana ya nguvu za rais.
"Mkuu wa Mkoa wewe ni dokta, unafahamu maana ya neno People, yaani ni watu, mimi ninawapongeza sana hawa wanaosema ‘Peoples Power’, kwani neno People ni watu ambao ndiyo Watanzania waliomchagua Rais Kikwete, na Power ni nguvu, hakuna mwenye Power kama rais, maana ya Authority ni Rais Kikwete ambaye ndio tunapata miradi mbalimbali ya barabara, miradi ya umeme na Big Results Now, kwa hiyo mimi ninawapongeza sana wale wanaosema Peoples Power," alisema Magufuli.
Akizungumzia juu ya nidhamu ya fedha, Magufuli alisema kumekuwa na matumizi yasiyostahili kwa baadhi ya Halmashauri juu ya fedha za miradi ya barabara, ambapo wakurugenzi hutumia fedha hizo kulipana posho za vikao.
Aidha Magufuli alisema Halmashauri zinapaswa kuibua vipaumbele na kuvitekeleza ili kupunguza changamoto za wananchi, na kwamba Mkoa wa Iringa utapatiwa zaidi ya shilingi Bilioni 5.6, ambazo zitasaidia kuboresha miundombinu ya barabara za wilaya katika mkoa huo.
Magufuli pia aliitaka Manispaa ya Iringa kubuni barabara za pembezoni ya mji na kujenga kituo kikubwa cha mabasi yaendayo mikoani.
Aidha Dk. Ishengoma alimuomba waziri huyo kulichukulia uzito suala la upanuzi wa barabara ya Mlima Kitonga, kwa madai kuwa ufinyu wa barabara hiyo umekuwa ukichangia usumbufu mkubwa pindi magari yanapokwama na hivyo kuziba barabara hiyo na kusababisha msongamano mkubwa.

Read more ...

Monday, September 16, 2013

Chadema kumshitaki Balozi wa China UN

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitamshitaki Balozi wa China nchini, Lu Younqing Umoja wa Mataifa (UN) kwa kukiuka Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa mwaka 1964 ambao unaeleza uhusiano wa kibalozi kati ya nchi na nchi.
Aidha, kimesema kitaiandikia barua Serikali ya China ili kutaka ufafanuzi kama imemtuma Balozi wake kufanya kazi ya uenezi siasa kwenye vyama.
Tukio la Balozi huyo kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CCM lilitokea Septemba tisa mwaka huu kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Wilaya ya Kishapu Shinyanga, ambapo Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana alimtambushisha balozi huyo huku akiwa amevaa sare za chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri kivuli wa mambo ya nje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana Jijini Mwanza, Ezekiel Wenje alisema Chadema wameamua kuchukua hatua hizo ili kukomesha vyama vya siasa kutumia mabalozi kama wawakilishi wa vyama vyao kwa kufanya uenezi kwenye mikutano ya siasa.
Wakati Wenje akisema hayo Katibu Mkuu Taifa wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema chama chake kinaangalia namna ya kumchukulia hatua za kumshtaki Balozi huyo akidai kuwa kitendo cha kushiriki siasa za CCM na kisha kuvalishwa kofia ya chama hicho ni kiunyume na taratibu za UN.
Kauli ya Dk Slaa aliitoa juzi jioni wakati akiwahutubia wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe.
Kiongozi huyo yupo mkoani Mbeya akiwa ameambata na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akifanya mikutano maeneo mbalimbali lengo likiwa kuwaeleza wananchi wa Mbeya kuhusiana na kitendo kilichomtokea Sugu na wabunge wengine bungeni hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Dk Slaa, balozi huyo alikiuka sheria na taratibu za Umoja wa Mataifa kwa kitendo chake ambapo alionekana kupanda kwenye jukwaa la mkutano wa CCM na kuvalishwa kofia ya chama hicho.
Kwa upande wake, Wenje alidai kuwa kwa mujibu wa mkataba wa Vienna Convention wa mwaka 1964 ambao unaeleza mahusiano ya kibalozi unakataza mabalozi kujingiza kwenye mambo ya ndani ya nchi ikiwa pamoja na kushiriki kwenye siasa.
“Mkataba wa Vienna Convention wa mwaka 1964 Ibara ya 41 kifungu kidogo cha kwanza kinakataza mabalozi kujiingiza kwenye mambo ya ndani ya nchi ikiwa pamoja na kufanya siasa.” alisema Wenje na kuongeza;
“Kitendo alicho kifanya balozi wa China kufanya kazi ya uenezi wa chama kimevunja mkataba huo jambo ambalo hatuwezi kulivumilia hata kidogo,”alisema.
Alifafanua kuwa licha ya Ibara hiyo kukataza jambo hilo Ibara ya 3 ya mkataba huo inataja wazi kazi wanazotakiwa kufanya balozi pindi anapokwenda kuwakilisha nchi yake sehemu nyingine.”alisema.
Source: Mwananchi
Read more ...

Thursday, September 5, 2013

Naibu Spika awaamuru Askari kumtoa mbowe nje ya bunge baadhi ya wabunge wapinga.

Vurugu kubwa zilizotokea Bungeni muda huu ambapo askari wa Bunge walikuwa wakivutana na Wabunge wa kambi ya upinzani waliokuwa wakipinga amri ya Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.

****
Vurugu kubwa zimetokea Bungeni hivi sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubaliana na amri hiyo.

Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo ni kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kusimama na kuanza kuzungumza pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali.

Mara baada ya zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi.
Read more ...

Tuesday, August 27, 2013

Zitto Kabwe aukataa Ubunge wala Urais 2015 Anataka awe......!


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.
Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.

Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).
"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.
Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani.
Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.
Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.
Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.
Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.

Source: Majira
Read more ...

Wednesday, July 31, 2013

SHEIKH PONDA ISSA PONDA APENDEKEZWA KUGOMBEA URAIS MWAKA 2015



Ikiwa  imebakia  miaka  miwili  kabla  ya  kufanyika  kwa  uchaguzi  mkuu wa  Rais  na  wabunge  hapa  nchini,baadhi  ya  waumini  wa  kiislamu  wameanza  kupendekeza  wagombea  wa  urais  wanaoona  kuwa wanafaa  ambapo  jina  la Sheikh  Ponda Issa Ponda  limeongoza....


Mapendekezo  hayo  yamedhihirika   katika  mihadhara kadhaa  anayoifanya Ponda  katika  mikoa  mbalimbali  nchini,ambako  amekuwa  akipendekezwa  na  kushauriwa  na  waumini  agombee  nafasi hiyo.....

Walianza  waumini  wa  msikiti  mkuu  wa  Ijumaa  wa  Arusha  alipokuwa  kwenye  ziara  mkoani  humo  ambapo  muumini  mmoja  alisimama  na  kusema  kwamba  kwa  mawazo  yake  anaona  Ponda  anafaa  kugombea  nafasi  ya  urais  kwa  vile  anaamini  kuwa  uwezo  wa   kuongoza  anao..

Alisema  mbali  na  uwezo pia  yuko  makini  katika  kusimamia  jambo lolote  lenya  maslahi  kwa  waislam  na  kwamba  mtu  wa  namna  hiyo  atafanya  vyema  zaidi  akipewa  dhamana  ya  kuongoza  nchi....

Inaelezwa  kuwa Ponda  alipotembelea  Zanzibar  alipata  wakati  mgumu  wa  kuwakataa  waislam  waliojitokeza   kumlaki  katika  misikiti  ya  Mpendae na  Mbuyuni  ambako  alifanya  mihadhara  na  kupendekezwa kugombea  urais  kwa  kura  nyingi  na  waumini  ....

Kufuatia  kusikika  kwa  mapendekezo  hayo,Kisiwa  lilimtafuta  Ponda  ili  kusikia  maoni  yake  juu  ya  maombi  ya  waislam  kumtaka  agombee  urais.

"Sikuwa  na  fikra  hiyo  hata  mara  moja,lakini  maadam limeletwa  nami  ni  kiongozi  wa  taasisi  ninawashukuru  waliofikiria  hivyo...

"Kwa  sasa  siwezi  kuzungumza  lolote  kuhusu  hilo, ntalifikisha  katika  taasisi  na  maulana  ndio  watakaolitazama  na  kutoa  uamuzi." Alisema  Sheikh Ponda

Ponda  alisema  kuwa  inawezekana  waumini  wakawa  na  mtazamo  huo  lakini  viongozi  wakawa  na  mtazamo  tofauti  kabisa,hivyo  akawataka  waumini  kuwa  na   subira  katika  hilo.
Read more ...

Thursday, July 18, 2013

Mwandishi Deo Balile ahojiwa na Polisi kwa 'Kufichua Ufisadi wamabilion' Ujio wa Obama.

 Wadau, safari ya kupambana na ufisadi katika nchi hii ni ngumu sana. Leo kuanzia saa 5 hadi saa 8:30 mchana, Mhariri Mtendaji wa Jamhuri, Deo Balile, amehojiwa Makao Makuu ya Polisi kuhusu habari iliyochapishwa kwenye Jamhuri inayohusu "Ufisadi ujio wa marais 11".
Kwa bahati nzuri, habari nzima wanaikubali kwamba ni ya kweli! Kasoro pekee eti ni matumizi ya barua ya Ikulu iliyokuwa na neno "Secret" ambayo ilikuwa na majina tu. Anashitakiwa kwa kosa la "Kuchapisha Nyaraka za Siri", jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Usalama, kifungu 5(1). Nimemwekea dhamana hadi Ijumaa saa 4 asubuhi.
Hii ndio habari Iliyosababishwa kuhojiwa hii hapa

Ufisadi wa kutisha ujio marais/Obama: Zaidi ya Bilioni 8 zatumika!

  • Hazina yatumia Shilingi bilioni 8
  • Wajanja’ watafuna mamilioni
  • Vifaa vya Obama vyaokoa jahazi
  • Vinyago vyagharimu Sh milioni 30
  • Sare, mikoba, vyagharimu mil. 400/-
  • Karamu, chupa za kahawa, miavuli mil. 390/-
  • Burudani ya muziki yatafuna milioni 195

Na Waandishi Wetu
Mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue), uliomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, umeigharimu Serikali Sh bilioni nane.


Hata hivyo, mamilioni ya fedha hizo yameishia mikononi mwa watumishi kadhaa wa Serikali kupitia zabuni tata walizotoa kwa kampuni mbalimbali.


Baadhi ya vifaa vilivyoorodheshwa kwenye zabuni hizo, ama havikuwasilishwa, au viliwasilishwa shughuli ikiwa imeshamalizika, na sasa vimetunzwa kwenye maghala. Miongoni mwa vifaa hivyo ni shehena kubwa ya bendera za Tanzania ambazo zimetunzwa katika chumba ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Wahusika wakuu kwenye ulaji huu ni maofisa kadhaa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa waliokuwa waratibu wa ugeni huo. Katibu wa Bodi ya Zabuni katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Onesmo Suka, ni miongoni mwa maofisa wanaokabiliwa na wakati mgumu kueleza mchanganuo wa zabuni ulivyokwenda.


Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umeonyesha kuwa kiasi hicho cha fedha cha Sh bilioni nane ni mbali kabisa na kile kilichokusanywa kutoka kampuni na mashirika mbalimbali ya umma.


Imebainika kuwa hadi Juni 5, mwaka huu, fedha taslimu zilizokusanywa ni Sh milioni 170 kutoka kampuni saba. Wachangaji wa kiasi hicho na kiwango kikiwa kwenye mabano ni Kampuni ya Simu ya Tigo (Sh milioni 80), PPF (Sh milioni 20), PSPF (Sh milioni 20) na LAPF (Sh milioni 20). Benki Kuu (BoT) ilitoa Sh milioni 10, Barrick Gold (Sh milioni 15) na Benki ya Azania (Sh milioni 5).


Kampuni tatu zilikubali kutoa vifaa. Vodacom iliamua kuchangia masuala ya ICT, Masasi Foods walitoa maji ya kunywa, ilhali Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) lilitoa fulana na zawadi ndogo ndogo.


Hadi Juni 5, mwaka huu, kampuni tano zilikuwa zikisubiri uamuzi wa Bodi. Kampuni hizo ni Mac Group, CBA Bank, PBZ Bank, Nokia-Siemens na Shirika la Hifadhi la Taifa (NSSF).


Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa kampuni nne zilishindwa kuchangia kwa kile kilichoelezwa kwamba ni uwezo wake mdogo kifedha. Kampuni hizo ni TanzaniteOne inayochimba tanzanite Mererani; IBM, Infrotech ba Diamond Trust Bank.


Wafanyabiashara nguli nchini hawakuachwa nyuma kwenye michango hiyo, ingawa taarifa zinasema wapo waliokataa kutoa. Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote, Balozi Ombeni Sefue, aliagiza wafanyabiashara kama Said Bakhresa na Mohamed Dewji wafuatiliwe kwa karibu ili waweze kutoa michango.


Hata hivyo, aliyekuwa Mkuu wa Sekretarieti ya Smart Partnership Dialogue, Victoria Mwakasege, anasema kwamba baadhi ya wafanyabiashara, wakiwamo kina Dewji, hawakuchangia. Hakutoa sababu za kushindwa kwao.


Sokomoko la matumizi mabaya ya fedha


Uchunguzi umethibitisha kwamba Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote, hakuridhishwa kabisa na namna zabuni zilivyotolewa.


Kwenye kikao cha mwisho, Sefue, kwa maandishi, alisema ingawa yeye ameshiriki katika Kamati ya Uendeshaji, hakubaliani na bajeti pamoja na mchanganuo wa zabuni ulivyokosa uwazi.


Sefue amenukuliwa akisema ni jambo gumu kwake kukubaliana na ununuzi huo kwa vile hapakuwapo mchanganuo wa kuthibitisha namna mamilioni ya fedha yalivyotengwa kuwalipa wazabuni na bei za vifaa vilivyohitajika.


Vyanzo vya uhakika kutoka ndani ya kikao kilichofanyika Juni 17, vinasema Balozi Sefue, aliweka wazi msimamo wake baada ya kuona taratibu za ununuzi zikiwa zimekiukwa, na kwamba baadhi ya vitu vilivyoorodheshwa, vilikuwa ni “vichekesho”.


“Mimi sitaki nihusishwe na jambo hili, waliolifanya wanapaswa wenyewe wabebe msalaba huu, mchanganuo uletwe ili kuonyesha nini kinanunuliwa kwa kiasi gani badala ya utaratibu huu wa kuorodhesha vitu na kuweka gharama,” alinukuliwa aking’aka Balozi Sefue.


Kampuni zilizopata zabuni


Mmoja wa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wamesema wazi kwamba fununu za kufanyika kwa mkutano wa Smart Partnership zilipoenea, watu wengi walipigana vikumbo wakitaka wapewe zabuni.


Kampuni ya Luma International Ltd ilipewa zabuni ya kusambaza vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni 391.1 Baadhi ya vitu hivyo ni vipeperushi, bendera za Tanzania (kubwa na ndogo), suti kwa watu wa protoko, sare kwa watu wa mapokezi, mabegi kwa wageni mashuhuri na wageni wa kawaida, na beji.Kampuni ya Softel Trading Company Limited ilipewa zabuni ya Sh milioni 392.6 kusambaza picha za mapambo ukumbini, miavuli (1,500), chupa za kahawa (800), vikombe vya kahawa (800), kalamu za zawadi (2,000) na vishikio vya funguo (800).


Kampuni hiyo hiyo ilipewa zabuni nyingine ya Sh milioni 48.25 kwa ajili ya kufanya kazi za usanifu kwa kutumia kompyuta na uchapaji wa mabango madogo madogo.


Kana kwamba haitoshi, kampuni hiyo hiyo ya Softel Trading Company Ltd ilipewa zabuni ya thamani ya Sh milioni 254 kwa ajili ya kutengeneza mabango makubwa 40. Wakati mkutano ukiwa unafanyika Dar es Salaam, iliamuriwa kwamba mabango hayo yasambazwe katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Zanzibar.


Kampuni ya Wild Cat Publishing ilishinda zabuni ya Sh 278,409,409,269 kwa ajili ya kuandaa machapisho 1,000 ya mkutano. Yalitakiwa yahusu masuala ya kiasiasa, kiuchumi, fedha, teknolojia, mawasiliano, usafirishaji, kilimo, ujenzi, afya na elimu, utalii, n.k.


Kampuni ya tano iliyoshinda zabuni ni ya Big Mama’s Woodworks ambayo ilipangiwa Sh milioni 29.96 kwa ajili ya kutengeneza zawadi za vinyago 60 yenye urefu wa sentimita 15 na upana wa sentimita 12 kila kimoja. Pia ilitakiwa itengeneze vinyango vinne vyanye urefu wa sentimita 150 na upana wa sentimita 35.


Kwenye masuala ya burudani, kampuni ya Prime Time Promotion ilijipatia zabuni ya Sh milioni 194.7. Kwenye orodha ya ugawaji zabuni, kampuni ya True Colour Entertainment Group ilizawadiwa zabuni ya Sh milioni 50 kwa ajili ya kuandaa na kuonyesha jarida. Ingawa haikufafanuliwa, hii yawezekana ndilo lile jarida lililoonyeshwa kwenye Ukumbi Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Smart Partnership. Lilihusu wanyamapori na vivutio kadhaa vya utalii vinavyopatikana hapa nchini.


Zabuni ya nane ilitolewa kwa kampuni ya Simply Computers (T) Ltd. Iligharimu Sh milioni 187.478. Ilitakiwa kusambaza kompyuta kubwa mbili, idadi kama hiyo kwa kompyuta za ukubwa wa kati na projekta nne.


Kampuni hiyo hiyo ya Simply ilipata zabuni nyingine yenye thamani ya Sh milioni 210.198 kwa ajili ya kusambaza kompyuta tano za mezani, laptop (5), laptop za sekretarieti na mkutano (14), mobile computing equipment (14), black and white printer (2), colored printer (2), kompyuta za mezani (nyingine 5), colored printer (nyingine 2) na flash disk (32).


Upungufu uliojitokeza


Pamoja na mamilioni hayo kupitishwa kwa ajili ya mkutano huo lakini bado kulikuwa na upungufu mkubwa katika utendaji hususani katika utoaji wa vitambulisho.vitabulisho wa


JAMHURI lilishuhudia baadhi ya wageni wakiwemo mabalozi kutoka katika mbalimbali Askari wa Jeshi la Polisi usalam wa taifa madereva wa Idara mbalimbalia za Serikali wakiendelea kusota kwa ajili ya kupata vitambulisho hivyo .


Kadhia hiyo pia ilimpata Katibu Mkuu Kiongozi, Sefue ambaye alifika katika Ukumbi wa Kalimjee saa nne asubuhi ambapo wafanyakazi wa waliokuwa wakihusika na utoaji wa vitambulisho hawakumjali jambo ambalo liliwasahangaza wengi waliokuwepo hapo.


Wengi wao walihoji uelewa wa wahudumu hao katika utendaji wao na kama kweli walikuwa hawamjui kiongozi huyo au ilikuwa ni dharau.


Sefue alikaa katika eneo hilo kwa zaidi ya nusu saa na kuondoka katika ukumbi huo huku akiwa hana kitambulisho hadi anaingia ukumbini wa Kimataifa wa Walimu Nyerere. Saa kumi jioni.


Wengine waliofika katika ukumbi huo na kupata kadhia hiyo ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana na mwenzake ambaye JAMHURI hailikufanikiwa kupata jina lake


Dk. Bana na mwenzake walifika na kujitambulisha kwa mmoja wahudumu katika ukumbi huo lakini mhudumu huyo baada ya kutekeleza shida yao, alianza kueleza matatizo yaliyoikumba idara hiyo ya vitambulisho.
“Jamani idara hii ina matatizo kwani hatukuwa tumejipanga kila mtu yuko kivyake ndio maana mnaona huduma imesimama kama mnavyoona hakuna majina hapa, mafaili yako tupu na wahusika hawapo kinachotakiwa ni kufika hapa na kuhakikisha jina lako na pia unakwenda kupiga picha pale lakini hadi sasa hatujapata majina je nyinyi mlijiandisha,” anasema mhudumu huyo.

Hata hivyo kauli hiyo ilimuudhi, Dk. Bana na mwenzake hivyo alimtaka mhudumu huo kutozungumza upungufu wa idara hiyo mbele ya wageni waliofika katika ukumbi huo, kwani kufanya hivyo ni aibu na haukuwa wakati wake kinachotakiwa kutoa vitambulisho.


Mhudumu huyo ambaye JAMHURI halikufanikiwa kupata jina leke alionekana kukerwa kauli hiyo aliendelea kuzumgumzia upungufu huo pamoja na Dk. Bana mwenzake kunyamaza. Waliondoka katika eneo hilo kwa miadi ya kurudi baadae.


Viongozi ‘warushiana mpira’


Utata kuhusu uhalali wa fedha zilizotumika kununua vitu hivyo, usiri kwenye utoaji zabuni na upungufu mkubwa uliojitokeza kwenye shughuli nzima ya mkutano huo, ni mambo yanayowasumbua sasa viongozi serikalini.


Wakati Katibu Mkuu Kiongozi akijitoa kwenye sakata hilo na kumsukumia Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule; Haule anasema yeye hahusiki. Badala yake anasema anayepaswa kuulizwa mambo yote yalivyokwenda ni Mkuu wa Sekretarieti ya Smart Partnership Dialogue, Mwakasege.


Kwa upande wake, Mwakasege anaruka kwa kusema Sekretarieti ambayo yeye alikuwa Katibu haikuhusika kwa namna yoyote na masuala ya zabuni. Akasisitiza kwa kusema, “Huyo anasema uniulize mimi (Haule), mwulize yeye. Mimi nilihusika na logistic, sisi tulipeleka mahitaji, kwenye zabuni hatukuhusika kabisa. Kilichofanyika ni sisi kukabidhiwa vitu kulingana na mahitaji. Yeye ndiye mwenye masurufu, ndiye anayejua hesabu zote za wizara.”


CHANZO: Gazeti JAMHURI

Read more ...
Designed By ApexbnewZ