Top News
Showing posts with label DailynewZ. Show all posts
Showing posts with label DailynewZ. Show all posts

Wednesday, August 13, 2014

Akamatwa Julias Nyerere Airport Na Madawa ya kulevya yaliokua kwenye nguo alizo vaa


Hati ya kusafiria ya mtuhumiwa huyo yenye namba AP816263 iliyotolewa Julai 3,2014 nchini Columbia. (picha: Francis Dande)


Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa akionesha Cocaine zilizokuwa zimefichwa katika mkanda wa suruali aliyokuwa amevaa raia wa Colombia, Andres Filipe Ballesteros Uribe (28), mara baada ya kukamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (picha: Francis Dande)


Suruali ya mtuhumiwa huyo ikiwa imezungushiwa Cocaine. (picha: Francis Dande)


Baadhi ya dawa alizokuwa amemeza mtuhumiwa huyo.


DAR ES SALAAM, Tanzania - KIKOSI cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kinamshikilia Andres Filipe Ballesteros Uribe (28) raia wa Colombia kwa tuhuma za kuingiza dawa hizo nchini kinyume cha sheria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa kikosi hicho, Kamanda Godfrey Nzowa alisema mtuhumiwa huyo aliingia nchini saa nane usiku kwa ndege ya shirika la Ethiopian akitokea Adisi Ababa.

Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na Cocaine iliyofungwa kwenye pakiti sita tofauti na kuiweka sehemu za siri, kiunoni kama mkanda na nyingine tumboni.

Kamanda Nzowa alisema mtuhumiwa huyo mwenye pasi ya kusafiria namba AP816263 iliyotolewa Julai 3,2014 nchini Columbia, alitoka Columbia kupitia Adis Ababa kuja Tanzania huku akibainisha kwamba hiyo ni njia mpya ya usafirishaji wa dawa hizo haramu.

“Hawa jamaa wanajaribu kubuni mbinu mpya kama huyu kijana alikuwa amefunga unga wa cocaine kama zilivyokuwa zikifungwa pipi na akazimeza… mpaka sasa ameshatoa pipi 13 kwa njia ya haja kubwa na anaendelea kutoa.

“…Sio rahisi kujua idadi ya mzigo aliokuwa nao mpaka atakapomaliza kuzitoa zote za tumboni ndiyo tunaweza kusema uzito wa dawa hizo na thamani yake,” alisema kamanda Nzowa.

Alisisitiza kwamba taarifa sasa wanazopeana kwenye mtandao wao unawezesha kukamatwa kwa watuhumiwa huku akibainisha kuwa lengo ni kudhibiti usafirishaji kwa njia yoyote.


Kamanda Nzowa alisema mafanikio yanaonekana kwa vile kuanzia Juni 24 mwaka huu hadi Agosti 10 hakuna mtu aliyekamatwa akiingiza huku akibainisha kwamba umadhubuti wa mtandao wao umefanikisha hilo.

“Asiyeamini kwamba tumefanikiwa atujaribu aone… naamini tunakokwenda dawa za kulevya hasa cocaine na heroine zitakuwa hazipiti wala kuingia Tanzania,” alisema na kuongeza kwamba wanadhibiti pia ulimaji wa bangi.

Kwa mujibu wa kamanda huyo lengo la mtandao wao ni kudhibiti sio kukamata wala kuteketeza.
Read more ...

Sunday, August 10, 2014

Picha: Serengeti Fiesta Mwanza CCM Kirumba Ilivyo Fana

 Kwa mara ya kwanza Fiesta mwaka 2014 imezinduliwa jijini Mwanza na hii ni baada ya miaka 10 tangu kuzinduliwa msimu huu ambao ilikuwa ni mwak 2004 na ilikua na slogan ya Utamaduni unaendelea.


 

























Picha kwa hisani Ya Makorokocho Blog.
Read more ...

Wednesday, August 6, 2014

Picha: AY ,D'Banj, Fall Ipupa wametembelea makao makuu ya benki ya dunia jijini Washington DC

Rapper Ambwene Yessaya aka AY aiwa na wasanii wenzake wa mradi wa One Campaign, jana wametembelea makao makuu ya benki ya dunia jijini Washington DC, Marekani.



Fally Ipupa, AY na D’Banj




AY aliongaza na D’Banj, Fally Ipupa na wengine.


“Kwanza jana tulikutana na wajumbe wa Youth African Leadership Initiative wale ambao walichaguliwa wakaja hapa kama miezi miwili hivi ambao kwa Tanzania kwa haraka haraka niliwaona ni mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari, Naibu waziri wa Nishati na Madini Steven Masele hao wawili niliwaona na watu wengine wa serIkali ya Zambia pamoja na viongozi mbalimbali wa nnchi za Afrika,” AY ameiambia Bongo5.


“Baada ya kukutana nao hapo sisi tukaenda kwenye rehearsal na introduction na baada ya hapo tukafanya rehearsal pamoja na wasanii wa Afrika ambao walikuja nahisi tulikuwa wasanii tisa au nane kwa sababu hatukuja wasanii wote ambao tulifanya ile project ya wimbo. Baada ya kumaliza ile function ambayo ilikuwa inafanyika white house watu wakaja kwenye ukumbi ambao ulikuwa unaitwa Newseum ambapo tukafanya kama after party tuka perform. Ilikuwa nzuri sana honestly,” ameongeza AY.


“Kwahiyo tukapiga fresh show nzuri sana, watu walifurahi sana. Tuliperform wimbo mmoja mmoja. Tukaperform mimi na Mwana FA, tukafanya Bila Kukunja Goti, tuliwachezesha mpaka wazee wazee ambao wapo kwenye serikali. Baada ya hapo tukaperform pamoja wimbo wa Cocoa na Chocolate then baada ya hapo ngoma ikawa imeisha. Leo (jana) hapa najitayarisha tunaenda World Bank na baada ya kwenda world bank halafu tutaenda Capital Center pia tutakuwa na meeting na watu ambao wana uhusiano na white house kwaajili ya kupitisha haya mabilioni kama ambavyo unaona wanayatoa kwenye CNN, Aljazeera na baada ya hapo kunaweza kukawa na after part nyingine I think baadaye kwaajili ya kuangana halafu kesho (leo) kila mtu anaweza kurudi kwake,” amesema.

Read more ...

Monday, August 4, 2014

Msimu mpya wa Serengeti Fiesta wazinduliwa

s1Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers SBL Bw. Ephraim Mafuru akizungumza na HAwahariri wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wakti wa uzinduzi wa Msimu mpya wa Serengeti Fiesta 2014 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki ambapo uzinduzi rasmi wa matamasha hayo utSerengeafanyika mkoani Mwanza tarehe 8 Agosti 2014 kauli mbiu ya Serengeti Fiesta mwaka huu ni “Sambaza Upendo” bia ya Serengeti ndiyo mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGAWE-DAR ES SALAAM)s2Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw Allan Chonjo akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo, kushoto ni Meneja wa bia ya Serengeti Lager Bwana Rodney Rugabwa.s4Mkurugenzi wa kampuni ya SCANAD Bi. Betty Addero Radier kulia akipozi kwa picha na Bw. Abdalla Singano Kampuni ya PR ya Abstract ya jijini Dar es salaam.s6Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers SBL Bw. Ephraim Mafuru kulia akizungumza na Mkurugenzi wa kampuni ya SCANAD Bi Betty Addero Radier kushoto na  Bw. Abdalla Singano Kampuni ya PR ya Abstract ya jijini Dar es salaam.s7Baadhi  ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyos9Baadhi ya waandishi wa habari wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo.s10Mhariri mkuu wa chumba cha habari Radio Clouds Bi. Joyce Shebe katikati akiwa na wanahabari wenzake wa Clouds Radio.s11Evance Mlelwa Mkurugenzi Masuala ya Kampuni akizungumza katika hafla hiyo.s12Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers SBL Bw. Ephraim Mafuru wa pili kutoka kulia  Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw Allan Chonjo kulia Evance Mlelwa Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni kushoto na Meneja bia ya Serengeti Lager Bw. Rodney Rugambwa wakionyesha bia za kampuni hiyo wakati wa hafla hiyo ya kuzindua msimu wa Serengeti Fiesta 2014.
Read more ...

Waziri mkuu mstaafu Mh Fredrick Sumaye Azindua Albamu mpya ya Rose Muhando Jijini Dar

  Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa albamu ya muziki wa Injili ,Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akionesha albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,mara baada ya kuizindua rasmi mbele ya maelfu ya washabiki na wapenzi wa nyimbo hizo za kiroho ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar jana.Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akifungua kasha lenye CD, wakati akizundua rasmi albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama sambamba na Mwimbaji nyota wa Injili,Rose Muhando wakishuhudia tukio hilo.Uzinduzi huo ulioandaliwa na kampuni ya Msama Promotions,ulionekana kufana kwa kwa kiasi kikubwa,huku waimbaji balimbali wakiwa wameshiriki onesho hilo,lililokonga washabiki na wapenzi wa muziki huo kwa kiasi kikubwa.Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akisalimiana na mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali. Baadhi ya Wadau wa Muziki wa Injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa. Sehemu ya umati ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Rose Muhanda akiwa na  skwadi lake jukwaani wakiimba mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani),wakati wa uzinduzi wa albamu yake mpya,uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hapo jana,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu  Mstaafu,Mh Frederick Sumaye. Rose Muhando akiimba kwa hisia Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria uzinduzi huo Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho,Upendo Kilahilo,akiimba jukwaani. Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya,Sara K akiimba Waziri Mkuu  Mstaafu,Mh Frederick Sumaye na wadau wengine wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya Rose Muhando iliyojulikana kwa jina la Shikilia Pindo la Yesu.
Read more ...
Designed By ApexbnewZ