Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini,
nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna
ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!!
Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake
mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha. Nikaegemeza maisha
yangu yote kwake.Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani
kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa
pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae?
Nilimkubalia kila kitu. Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu.
Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka
kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana.
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba
pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara ya kwanza nikatoa mimba. Haikuniuma
sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini
hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu.
Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na
nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa nawahi kulewa. Akautumia udhaifu huu
kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume
na maumbile. Alinilawiti!!
Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa
kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi. Mchezo
ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu
mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu.
Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona
katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa
mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa
ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na
atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile.
Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabakimwenyewe
katika msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi?
Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!! Nilijua tayari ameniacha!!!
Afya yangu ikadolola sana, nikalazimikakwenda
kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia. Siku zikasonga
nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau
yule aliyenitenda.
Nilipomaliza chuo akajitambulisha nyumbani na
alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili
na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa
hi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.
Nikaambiwa kizazi change kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia
mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa. Nililia sana huku
nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu
sahihi.
Nimekuandikia barua hii mdogo wangu.Uisome
mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu. Uwasimulie bila
kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya mambo magumu kuwaridhisha
wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliz a
usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote
kuhusu yule mumemdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa
sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana
hawa.
Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume
mwenzako AMENITENDA HIVI!!!
TAFADHARI TAFAKARI
Moja ya simulizi za kusisimua sana na yenye
kuleta hisia za aina fulani unaisoma. Hakika nilishindwa kubakia nyao kichwani
nilipokutana nao kupitia MORO NEWS Blog,
na nikaona si mbaya kushare na wadau hapa.
No comments :
Post a Comment