![]() |
Shamsa Ford |
VIDEO inayomuonesha msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford
akijifungua, imezua kizaazaa baada ya mtu asiyejulikana kuichukua bila ridhaa
ya mhusika na kuisambaza kwa watu mbalimbali.
Akizungumzia suala hilo hivi karibuni, rafiki wa
karibu wa Shamsa alisema kuwa, video hiyo ya msanii huyo ilirekodiwa kwa ajili
ya kumbukumbu zake, lakini
ameshangaa kusikia kuna baadhi ya watu wanayo.
“Yaani video hiyo imezua kizaazaa, Shamsa anahaha kumjua
aliyeisambaza lakini pia anahakikisha haiwafikiii watu wengine na vyombo vya
habari kwani inamuonesha hatua kwa hatua akijifungua,” kilisema chanzo hicho
Baada ya kuzipata taarifa hizo, this is diamond alimtafuta
Shamsa ambaye alisema:“Kiukweli nimeumia sana,
hiyo video ni kwa ajili ya kumbumbuku zangu, kwa nini mtu
aichukue na kuisambaza bila ridhaa yangu? Imeniletea matatizo makubwa.”
wameripoti mtandao wa this is diamond
No comments :
Post a Comment