Mkuu wa polisi wa eneo hilo Richard Bitonga
alisema mwanamume huyo alijitia kitanzi nje ya nyumba yake katika kituo
cha kibiashara cha Lwanda, eneo bunge la Nyatike.
“Alianza kwa kuvaa nguo ya chama cha ODM iliyokuwa
na picha ya Waziri Mkuu kabla ya kujitia kitanzi,” Alisema Bitonga.
Ingawa hakuacha ujumbe wowote, alikuwa amewaeleza marafiki wake kwamba
alikasirishwa na uamuzi wa mahakama.
Baadhi ya wakazi walisema marehemu alikuwa
ametisha kujitoa uhai ikiwa Odinga hangeshinda kesi ya kupinga uchaguzi
wa urais. “Alisema hakuona sababu ya kuendelea kuishi katika ulimwengu
huu ikiwa Odinga hatakuwa Rais wa nchi hii,” alisema mkazi Samuel
Otieno, ambaye ni mchimba dhahabu.
Mbunge wa eneo hilo, Eric Anyanga alisema
“Uamuzi wa mahakama ulishtua wafuasi wengi wa Cord kote nchini
waliotarajia awamu ya pili ya uchaguzi wa urais baada ya dosari tele
kugunduliwa katika uchaguzi wa Machi 4,” alisema Mbunge huyo
Wakati huohuo, Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu
wa Rais Kalonzo Musyoka wanapanga kukutana na maseneta na Wabunge wa
Muungano wa CORD wiki ijayo kujadili hatima yao ya kisiasa baada ya
uchaguzi mkuu kukamilika.
Odinga na Musyoka walikutana na baadhi ya wabunge
na maseneta wa Cord katika ofisi ya waziri mkuu katika barabara ya
Harambee Avenue, Nairobi.
No comments :
Post a Comment