Gichana ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu
nchini Kenya, alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana na kusomewa
mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Osward Tibabyekomya, akisaidiana na
Wakili wa Serikali Tumaini Kweka.
Akisoma mashtaka mshtakiwa huyo, Wakili Oswald
alidai kati ya Novemba 2009 na Agosti 2010 jijini Nairobi, Kenya;
Arusha na Dar es Salaam, nchini Tanzania, akiwa na washtakiwa wengine
ambao hawapo mahakamani walikula njama za kutenda kosa la kutakatisha
fedha haramu.
Wakili Oswald alidai kuwa mshtakiwa huyo pamoja na
wenzake walitenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 12 cha Sheria ya
Kuzuia Utakatishaji Fedha Haramu, namba 12 ya mwaka 2006.
Katika shtaka la pili, anadaiwa kutenda kosa la utakatishaji fedha. Anadaiwa kuwa kati ya Novemba 2009 na Agosti 2010 kwa kupotosha ukweli wa chanzo cha fedha alizokuwa nazo, alizihamisha kutoka Kenya kwenda Arusha na kisha Dar es Salaam.
Katika shtaka la pili, anadaiwa kutenda kosa la utakatishaji fedha. Anadaiwa kuwa kati ya Novemba 2009 na Agosti 2010 kwa kupotosha ukweli wa chanzo cha fedha alizokuwa nazo, alizihamisha kutoka Kenya kwenda Arusha na kisha Dar es Salaam.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuhamisha fedha hizo kwa
kutumia hundi yenye thamani ya Dola za Marekani 4,940,363.25, ambazo
anadaiwa kuwa aliziweka katika akaunti namba 02J1036325000 inayomilikiwa
na Kampuni ya Moyale Precious Germs Enterprises katika Benki ya CRDB
Tawi la Meru, Arusha.
Wakili Oswald alidai mahakamani hapo kuwa baadaye
mshtakiwa huyo alihamisha tena fedha hizo kutoka Tawi la Meru, Arusha
kwenda Makao Makuu ya Benki ya CRDB Dar es Salaam, kwa nia ya kufanya
utaratibu wa kuzitoa, huku akijua hundi ilikuwa ya kughushi. Hakimu
Emillius Mchauru alisema kesi itatajwa Aprili1 Aprili 18 .
No comments :
Post a Comment