Hata hivyo kuna ukweli katika maisha ya sasa kuwa
watu kutoka baadhi ya mataifa wakiwa wamekula chumvi nyingi zaidi na
kuingia katika vitabu vya historia.
Wilayani Mpwapwa kuna mfano mzuri na ambao uko
wazi, kwani yuko mwanadamu mwenye umri wa miaka 113 ambaye anaishi hadi
sasa na anakula vyakula vyote wanavyokula wengine ikiwemo vitu vigumu
kama nyama.
Ni katika Mtaa Igovu Kitongoji cha Ng’ambo si
mbali kutoka katika makaburi ya wakoloni walioishi Mpwapwa zama hizo,
katikati ya nyumba nyingi zilizojengwa kwa matofari ya udongo yupo Bibi
ambaye ni maarufu kwa jina la Mdala Aksa liyezaliwa mwaka 1900.
Aksa au Nyamiti (jina la utoto) ni mzaliwa pekee
katika familia ya Marehemu Luwaha pamoja na mkewe aliyeitwa Mkaulugu
wote wenyeji wa Mkoa wa Iringa, ingawa yeye anapinga kuwa si Iringa bali
ni Uheheni.
Simulizi zinaonyesha kuwa familia hiyo ilikuwa na
ukaribu sana na familia ya shujaa na mtemi wa wahehe Mkwawa ambaye ni
mtoto wa Muyugumba.
Bado anaweza kuzungumza na kusikia bila ya shida
yoyote lakini kinachomsumbua ni macho kupungua uwezo wa kuona, pamoja na
miguu yake kukosa nguvu ingawa anaweza kutembea kwa msaada. Muda mwingi
maisha ya mama huyo ni kulala tu.
Ndani ya nyumba
Nilipoingia ndani ya nyumba nilipata kusikia
mambo mengi, kwanza ni historia ya kikongwe huyo ambaye licha ya
kupoteza baadhi ya kumbukumbu, anaonyesha mwenye uelewa mkubwa na
masikio yake yanasikia kwa ufasaha na umakini wa hali ya juu.
Simulizi yake
“Zinji semigwe ninga……”(mengine nimesahau ila…….)
anavuta pumzi na kuanza kusimulia kuwa alizaliwa mkoani Iringa baba
yake akiwa ni mhehe na mama yake alikuwa ni mgogo mwenye mchanganyiko wa
wahehe na alizaliwa akiwa pekee, kutoka kwa mama yake Mkaulugu.
No comments :
Post a Comment