Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa
dhamana jana jioni ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa
Lema wakili Humphrey Mtui
i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi
wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote
ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la
msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)
ii)Kosa la pili
ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu
na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile
anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali
matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi
iii)Kosa la Tatu
ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo
sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa
kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini
kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa
mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa
kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa
katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni
kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni
uchochezi.
Maneno ya hapo juu ndiyo yaliyosababisha jeshi
la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane ....
Huo
umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi
kupitia simu yake kupitia namba 075296027* aliyotishia kumbambikizia
kesi anayoitaka yeye.
No comments :
Post a Comment