Top News

Thursday, April 4, 2013

HII NDIO FILAMU ILIYO ZUIWA KWA KUUZALILISHA UKATOLIKI

Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.

 

Filamu Sister  MARRY iliyokua ikisubiriwa na wapezi wengi wa filamu za hapa nyumbani (Bongo)  imemuwia ngumu muigizaji Ray ngumu kuitoa kutokana na masharti aliyopewa na uongozi wa kanisa la Katoliki wakidai kua inadhalilisha ukatoliki katika baadhi ya vi pande.
 Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. “Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ