Akizungumza jana, Aboubakar (26) alisema hotuba ya
Rais Jakay Kikwete ilimgusa na alipata hamasa ya kusaidia watu
waliokuwa wamenaswa ndani ya kifusi.
“Nilifika eneo la tukio saa 3:30 asubuhi baada ya
kupata taarifa za maafa hayo katika vyombo vya habari. Nikakimbia mara
moja kuja kusaidia,” alisema Aboubakar.
Kijana huyu, ambaye hajawahi kusoma shule ya msingi au sekondari ingawa alipata mafunzo kidogo ya uokoaji.

Alisema alipofika eneo la tukio aliomba kuendesha
kijiko kilichokuwa kunatumika kwa uokoaji, lakini raia na baadhi ya
wanajeshi walimcheka, hakujali.
Alisema aliporuhusiwa alianza kazi na ilipofika
saa 8:00 mchana alikuwa wa kwanza kuibua mwili wa kwanza ambao ulikuwa
wa mwanamke.
“Ukiniuliza… hata cheti cha darasa la saba sina. Lakini ninajua vitu vingi,” alisema Aboubakar.

Uwezo wa kipekee
Shafii Khalifa, ambaye ni mtu mwingine aliyejitolea kuokoa, alikiri Aboukabar kuwa na kipaji cha ziada cha uokoaji tofauti na wengine.
“Alikuwa anaelekeza tu, ukienda hapo kweli unakuta mwili,” alisema Khalifa.
Khalifa alisema waokoaji wengine walimdharau wakidhani labda ni mwendawazimu, lakini baadaye alikuwa msaada mkubwa katika zoezi zima.

“Hajalala tangu Ijumaa, amekuwa hapa hadi leo (jana) tulipomaliza uokoaji,” alisema.
Aboubakar alisema mwili wa mwanamke huyo ambaye ni mama lishe aliyekuwa akifanya shughuli zake mbele ya jengo hilo, ulikuwa umepasuka tumbo na utumbo wote ulikuwa nje.
Aliendelea kusimulia, ilipofika saa 1:00 usiku aliweza kuopoa miili mingine mitatu na usiku wa manane, miili mingine miwili ilipatikana.

Usiku wa kuamkia jana, miili mingine minne iliyoopolewa na Aboubakar kutoka eneo la varanda ya jengo hilo.
Namna ya kugundua maiti
Aboubakar, mkazi wa Magomeni Kagera, amekuwapo eneo hilo tangu Ijumaa saa 3:30 usiku hadi jana saa 4:00 mchana wakati zoezi linamalizika. Alihusika moja kwa moja na kuopoa miili yote 36 iliyokuwa imefukiwa na kifusi.

“Nina uwezo wa kunusa harufu katika kifusi na
kujua kama kuna mwili au la. Cha muhimu ni kumwagia maji juu ya kifusi
na unaipata harufu,” alielezea kipaji hicho.
Alisema ili kujua iwapo kuna maiti katika mchanga,
unamwagia maji juu ya kifusi, kisha unaifuata harufu ya vumbi
inapoelekea na utajua iwapo eneo hilo lina mwili au la.
Aboubakar alisema aliwahi pia kusaidia kuopoa miili ajali ya meli ya Mv Skagit, visiwani Zanzibar.

Alisema katika maiti zote 36, wanawake walikuwa watatu, mamalishe wawili na mwanamke mmoja ambaye anaonekana alikuwa mpitanjia.
No comments :
Post a Comment