Top News

Friday, April 26, 2013

KIJANA WA CHADEMA BEN SAANANE ANARIPOTI,DR.SLAA AFUATILIWA NA WATU,ATAJA NAMBA ZA GARI NA TUKIO ZIMA

Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.
Dr.Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri

Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr.Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG.Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo
Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo

Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi?Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi?Mambo haya ni bora yafahamike mapema na
watanzania wayajue.Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa

Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala.Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ