Ni wakati wa kuahirisha kikao cha leo asubuhi dakika tatu zilizopita.
Kulikuwa na msuala matatu yaliyojitokeza bungeni moja la Waziri kuja
bungeni na kutoa kauli ya serikali kwa mdomo bila kuwa na maandishi kama
inavyotakiwa na kanuni.
Suala jingine ni la mabadiliko ya utaratibu wa kupitisha vifungu bunge
litakapokaa kama kamati. Maswali kuhusu hili yalijikita kwenye ukweli
kwamba hakuna document yoyote iliyoletwa na hivyo itakuwa hawajui ni
kifungu kipi kinapitishwa na hivyo serikali irudi tena ije na documents
kama inavyotakiwa.
Swali la Waziri kutokuja na document liliulizwa na Zitto Kabwe na baaday
msisitizo ukawekwa na Tundu Lissu kwa kutaja kanuni 49(3) isemayo hivi:
{Waziri mwenye kutoa kauli atawajibika kutoa nakala ya kauli yake kwa Wabunge wote wakati anapoiwasilisha Bungeni.}
Wakati swali la serikali kutakiwa kuja na document kwa ajili ya Kamatiya matumizi liliulizwa na John Mnyika.
Spika alipoinuka alikubaliana na swali la kwanz akwa Waziri kwamba
waliamua Waziri aje kwanza atoe kauli ya mdomo lakini himazuii kutoleta
statement na hivyo atahitajika kuileta ili isiishie kuwa ya mdomo.
Kuhusu swali la Mnyika, Spika alisema lilikuwa ni swali obvious na
angeshangaa kama wabunge wasingeuliza. Na akataja kwamba sababu ni
kwamba utaratibu huu ndio mara ya kwanza unatumika na hivyo estimate ya
muda ilifanya ifanyike hivyo. Lakini amekiri kwamba kabla ya kukaa kama
kamati ni lazima watoe documents watakazogawiwa wabunge.
MY TAKE:
Tumeona Spika akisema kuwa angeshangaa kuona kama wabunge wasingeuliza
maswali hayo ya msingi. Pia amekubaliana nao. Lakini wasingeuliza ili
kutimiza mshangao wake basi hatujui ingekuwaje na huenda ingekuwa kama
ilivyoelekea kuwa.
Sasa, kama Spika alijua kuwa haya ni maswali ya msingi na ya kikanuni,
hebu angalia walioyauliza (Zitto, Tundu, Mnyika). Wote ni Chadema.
Utaachaje kusema kwamba alichotarajia hoja y amsingi kama ile isiulizwe
na wabunge kwa kweli kwa namna moja ni sawa na yeye kujua kwamba
haiwezekani hoja ya msingi ipite kimya mle bila Chadema kuuliza.
Hakuna CCM hata mmoja aliyeinuka kusema lolote katika haya ambapo yasingesemwa yangepita hivihivi tu kama ilivyoelekea.
No comments :
Post a Comment