Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mkumbukwa Joseph.
Hata hivyo, mazishi hayo yaliathiriwa kidogo na mvua iliyofanya baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki washindwe kuuaga mwili wa marehemu.
Watu wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Josephat Mkumbukwa. Kushoto ni mjomba wa marehemu Erasto Kombe.
Mkumbukwa alifariki China na maiti yake
kuhifadhiwa hospitali kwa takriban mwaka mzima na serikali ya nchi hiyo
huku mkewe, Neema Majukano pamoja na rafiki wa marehemu aitwaye Haji
Msongore wakilaumiwa kwa kushindwa kutoa taarifa mapema juu ya kifo
hicho.
Paroko wa Kanisa Katoliki Kigango cha Mabatini Nyamagana, Charles Bundu, akiendesha ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Joseph Mkumbukwa aliyeuwa nchini China mwaka jana.
Aidha, utata umegubika kifo cha Mkumbukwa
kufuatia rafiki huyo wa marehemu ambaye mara ya mwisho walikwenda wote
nchini Chini kudaiwa kumuoa mke wa marehemu, Neema.
Source GPL
No comments :
Post a Comment