Thursday, June 19, 2025

Wednesday, April 24, 2013

UNYAMA WAKUTISHA: HIVI NDIVYO ALIVYO CHOMWA KISU MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA IAA:

 

Picha  ya  marehemu  Henry Koga  baada  ya  kuchomwa  kisu  na  kufariki  hapo hapo  jana  usiku  katika  chuo  cha  uhasibu  Arusha.....


GODBLESS LEMA ANASAKWA
VIKALI NA JESHI LA POLISI KWA
UCHOCHEZI NA UANZILISHI WA VURUGU
ZA CHUO CHA IAA ARUSHA LEO...!! Baada ya mkuu wa mkoa kufika eneo la
tukio aligoma kuzungumza na wanafunzi
hao, akidai kwamba hawezi kuongea
mpaka Mh.Lema aondoke, ndipo
atapanda kuzungumza na pia alilalamika
kwamba hamna kipaza sauti kwa hiyo hawez kupaza sauti yake kuzungumza
na watu wasio na nidhamu. Maneno hayo yalipandisha hasira ya
wanafunzi hao lakini walitulizwa, na
kipaza sauti kikaandaliwa katika ukumbi
wa chuo maaruf kama "main cafetaria"
ili mkuu huyo azungumze. Wanafunzi walikusanyika eneo hilo
kumsikiliza lakini alivyoanza kuongea,
wanafunzi walisikika wakimzomea kwa
madai kwamba ameonesha dharau. Wanafunzi walianza kuzomea na
kumrushia chupa zaa maji na mawe
mkuu wa mkoa na hapo ndipo ilibidi
mabomu ya machozi yatumike
kuwatuliza wanafunzi wa chuo hicho. Kwa muda wa masaa mawili imekuwa
ikisikika milio ya mabomu chuoni hapo
mpaka hali ilipo tulia kabisa. Kwa sasa hali ni shwari chuoni hapo ila polisi wametapakaa huku na kule wakisema wanamtafuta Mbunge wa jimbo la Arusha kwa madai kuwa ndiye anaye chochea mgomo huo wa wanafunzi. Mbunge huyo alikimbia kuelekea kusikojulikana na kutelekeza gari yake chuoni hapo, ambayo polisi walilazimika kuivuta kwa "breakdown" car kuelekea kituo cha polisi. kama inavyoonekana katika picha. Gari ya Mh.Godbless Lema ikiochukuliwa
na polisi kutoka eneo la tukio Polisi wakichukua gari ya mbunge wa
jimbo la Arusha Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha
kililazimika kutumia Mabomu ya Machozi
kuwatuliza wanafunzi waliokuwa
wakishinikiza kuandamana baada ya
mwanafunzi mwenzao kuuawa kwa
kuchomwa kisu na watu wasiojulikana majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo. Tukio hilo liliamsha hisia za wanafunzi
hao na kuwafanya wakusanyike
kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa
Arusha kwa madai kwamba matatizo
yao huwa hayafikishwi ipasavyo, hivyo
wanataka kuyawasilisha wenyewe. Juhudi za uongozi wa chuo kuwatuliza
wanafunzi hao zilishindikana, na
ilipofika majira ya saa nne asubuhi,
Mbunge wa jimbo la Arusha alifika katika
eneo hilo kuwasikiliza wanafunzi hao. "Tunatoa dakika thelathini mkuu wa mkoa awe ameshafika hapa, kama
hajafika ndani ya muda huo,
tunaandamana wote, mimi mbele nyie
nyuma mpaka ofisini kwake" alisema Mheshimiwa Lema

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ