Katika utafiti uliochapishwa kwenye gazeti la Science watafita wa maabara ya ATR Computational Neuroscience ya mjini kyoto, magharibi mwa Japan walitumia scanner za magnetic resonance imaging (MRI) kubainisha ni sehemu gani kwenye ubongo unaokua ukifanya kazi mtu anapokua usingizini.
Wanasayansi hao kisha waliwaamsha waotaji kisha kuwauliza picha walizoziota mchakato ambao ulirudiwa mara 200
Majibu hayo yaliunganishwa na ramani za ubongo zilizo tengenezwa na Scanner MRI na kisha walitengeneza database kulingana na majibu
Katika majaribio yaliofuata waliweza kubashiri picha zipi walizoziona watu waliojitolea na ambao walipata jibu la uhakika kwa asilimia 60
Timu yake kwa sasa inajaribu kubashiri mambo mengine ya ndoto ikiwemo harufu, rangi mawazo na pia story inzima ya ndoto za watu. Hata hivyo mtafiti mkuu wa maabara hiyo Yukiyasu Kamitani alikiri kua bado kunasafari ndefu mpaka waielewe ndoto nzima
Utafiti huo ulutumia tu picha walizoona watu hao muda mfupi kabla hawajaamshwa ambapo katika usingizi foofofo mtu huwa na ndoto ambazo imebaki fumbo
Bado kuna mambo mengi yasiojulikana, Aliliambia shirika la habari AFP
No comments :
Post a Comment