Zitto pia amemwomba Cameron kuzishawishi nchi
nyingine tajiri kuwa na sheria za aina hiyo ili kudhibiti mafisadi wa
nchi zinazoendelea.
Hatua hiyo ya Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema upande wa Tanzania Bara, ni mwendelezo wa juhudi zake za
kupambana na mafisadi ndani ya Serikali wanaodaiwa kuweka katika benki
za nje kiasi cha dola za Marekani milioni 196 (sawa na Sh323 bilioni).
Zitto amechukua hatua hiyo kwa kuzingatia kuwa
Waziri Mkuu Cameron atakuwa mwenyeji wa Kundi la Nchi Tajiri Duniani
linalojulikana kama G-8 ambalo litakutana Lough Erne, Uingereza kuanzia
Juni 17–18. Cameron ndiye atakuwa Mwenyekiti wa mkutano huo.
Novemba mwaka jana, Mbunge huyo alipeleka hoja
binafsi bungeni akitaka iundwe timu maalumu kwa ajili ya kufuatilia
kiasi cha Sh 323 bilioni ambazo zimethibitika kufichwa Uswisi.
Zitto aliikabidhi barua hiyo Jumatatu ya wiki hii
kwa Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose, akimwomba aiwasilishe kwa
Waziri Mkuu Cameron, kuelezea kilio cha Watanzania kuhusiana na fedha
hizo.
Alisema sheria hiyo ina athari kubwa kwa maisha ya
Watanzania wengi maskini na Afrika kwa ujumla, ambapo alisema anaamini
sheria inayotaka uwazi itapitishwa kwenye mkutano wa mataifa manane
tajiri yenye viwanda duniani, maarufu G-8, utakaofanyika mwezi ujao.
Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Fredrick Werema alisema kuwa ana taarifa kuhusu barua
hiyo iliyoandikwa na Zitto kwenda kwa Cameron kuhusu shinikizo la
Serikali kufanya mchakato wa kurudisha fedha zilizofichwa nje ya nchi.
“Tunafanya kazi na siyo kuzungumza ovyo kila
mahali au kila hatua tuliyofikia, ila tunafanya kazi masaa yote,
Watanzania wasubiri tu hatua tutakayofikia na tukiona tumejiridhisha
tutawaambia nini kimefanyika,” aliongeza Werema.
No comments :
Post a Comment