Mh Lema amethibitisha ya kwamba ushahidi alioagizwa kuuwasilisha kwa
spika wa bunge ya kwamba Rais Jakaya Kikwete ni kinara wa udini tayari
ameshaukamilisha.
Aliyasema haya hapo jana nilipokuwa nikizungumza naye ya kwamba
aliamriwa kuuwasilisha katika vikao vya bunge vya wiki hii lakini
akashindwa kufanya hivyo kutokana na uhuni wa jeshi la polisi nchini na
idara ya usalama wa Taifa pamoja na uhuni wa anayejitambulisha kama mkuu
wa mkoa wa kumkamata kama jambazi na kumuweka rumande kwa muda wa siku
nne.
Lakini alisema tayari ameshamuandikia barua spika wa bunge ya kumtaarifu
kilichotokea Arusha na kwamba ushahidi wake umeshakamilika na yuko
tayari kuuwasilisha katika vikao vya bunge vya wiki ijayo.
Akidokeza juu ya ushahidi huo alisema uko katika video na nyaraka
mbalimbali za maandishi ambapo kama spika ataridhia uwasilishwe ndani ya
bunge basi chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na chama kimoja cha
upinzani vitaenda kufa kabisa kutokana na ushiriki wake katika udini
huo. Lakini akasema endapo spika wa bunge ataamua kufanya uhuni wa
kutoupeleka bungeni kama alivyofanya katika ushahidi wake ya kwamba
WAZIRI MKUU NI MUONGO basi atakiomba chama chake kikubali ushahidi huo
uwekwe katika mitandao ya kijamii pamoja na youtube ila kila Mtanzania
na wasiokuwa watanzania waweze kuona Rais anavyoligawa Taifa la
Tanzania.
Alisema kutokana na usalama wa ushahidi huo ameamua kumuita Arusha
katibu wa Chadema mkoa wa Dar es salaam bwana Henry Kilewo kwa ajili ya
kuuchukua na kuupeleka Dar ambapo utapelekwa Dodoma. Na tayari bwana
Kilewo ameshauchukua na kuupeleka Dar kwa ndege ya fast jet iliyoondoka
jana usiku saa tatu. So jumapili mh Lema atakapokuwa anaelekea Dodoma
atakuwa hajabeba ushahidi huo bali ataukuta Dodoma.
Pia katika video hiyo yumo shekh Ilunga wa Morogoro akifanya vikao na
viongozi hao ( Rais pamoja na kiongozi huyo mkuu wa chama cha upinzani)
Ifike wakati tatizo lijulikane liko wapi na kutafutiwa ufumbuzi
ReplyDelete