Mchungaji Msigwa katika uchangiaji katika kikao cha Asubuhi
ameongea kwa uchungu sana kuhusu jinsi rasilimali za nchi hii
zinavyoteketezwa kwa manufaa ya watu wachache.Ameshangazwa sana na
Kitendo cha waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Nchimbi kwa kuendelea
kutetea ujangili kwa ngonjera baadala ya kumtaka Msigwa alete ushahidi
ili yeye kama waziri aliyepewa zamana kuchukua hatua stahiki kwa
watuumiwa.Ila ashangai Coz Nchimbi alianza kuitwa Dr. kabla ya kuwa Dr.
Kuhusu Mgogoro wa Loliondo anasema inashangaza Waziri anateuliwa na
Raisi,Katibu Mkuu wa CCM anateuliwa na Raisi iweje jambo ambalo
limetolewa uhamuzi na waziri likachunguzwe na hao wateule wengine wao
Rais? Hili linaonyesha udhaifu katika taasisi ya Raisi.
Uwezo wa CCM kutataua mgogoro huu ni mdogo sana kwasababu wao ndiyo
waliutengeneza tangu enzi za mwinyi.Baada ya yeye kusoma hotuba yake
amekuwa akipokea simu(Private Number) zikimtisha kwa kushikia bango
issue ya Tembo.
No comments :
Post a Comment