Polisi
nchini Tanzania inawashikilia watu wa nane kwa madai ya kuhusika na
mlipuko wa siku ya jumapili katika kanisa Katoliki la Olasit viungani
mwa mji wa Arusha.
Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa Tanzania.
Wakati mwandishi wa BBC Baruan Muhuza akuzungumza akiwa
hospitalini mjini Arusha amesema idadi ya watu waliofari dunia kufuatia
mlipuko huo ni wawili na wala sio watatu kama ilivyoripotiwa hapo awali.
Polisi mjini Arusha vile vile wamethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio hilo la kigaidi ni wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza ni kulipuzi aina gani kilitumika wakati wa shambulizi hilo.
Lakini Baruan Muhuza ambaye alitembelea eneo la tukio mbali na majeruhi
hakuna hasara kubwa iliyotokea mahali hapo pia sakafi na kuta za kanisa
hilo hazikuchimbika sana.
Kutoka Dar es Salaam Leornad Mubali anaongezea kuwa watu wawili
sana wamethibitishwa kufariki dunia katika mlipuko huo uliotokea majira
ya saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya mji
wa Arusha nchini Tanzania na wengine kadhaa kujeruhiwa huku balozi wa
papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya uzinduzi wa
parokia mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi wakinusurika pia .
Kwa mjibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa
katoliki jimbo la Arusha mlipuko huo unapotokea walikuwa tayari katika
hatua ya kubariki maji kwaajili ya uzinduzi wa kanisa ulikuwa ukiongozwa
na balozi wa Papa Fransis.
Shambulizi la Arusha
Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa taarifa walizonazo muda
mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali watu kati yao wamefariki
huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mount
Meru mjini Arrusha.
Shughuli zote kuhusiana na ibada hiyo zimesitishwa huku watalaalamu wa
milipuko na polisi wakiendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.
Bado hakuna taarifa zozote kuhusiana na chanzo halisi cha bomu hilo ama
kundi lolote linalodaiwa kuhusika na utegaji wa bomu hilo.
Hili ni shambaulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japo kuwa mwaka huu
pia kulikuwa na mtukio ya mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani
Zanzibar ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia
kanisani.
No comments :
Post a Comment