Rama na mama yake walikuwa wakikabiliwa na shtaka
moja la kumuua kwa makusudi mtoto Salome Yohana (3), kinyume cha kifungu
cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Hata hivyo, jana Mahakama Kuu ilimwachia huru Rama
baada ya kuridhika na ripoti ya jopo la madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa akili yake, iliyoeleza kuwa wakati wa tukio hilo hakuwa na
akili timamu.
Wakati Rama akiachiwa kwa kutokana na ripoti hiyo
ya madaktari, mama yake aliachiwa huru baada ya upande wa mashtaka
(Jamhuri) katika kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2010, kudai kuwa hauna nia
ya kuendelea kumshtaki.
Kuachiwa kwa washtakiwa hao kulisababisha vilio
kwa mama wa mtoto aliyeuawa, Upendo Dustani na shangazi wa mtoto huyo,
Furaha Mussa, aliyekuwa akiishi na mtoto huyo nyumbani kwake Tabata.
Septemba 29, 2011, Mahakama Kuu iliamuru Rama
apelekwe katika hospitali ya magonjwa ya akili ili apimwe akili kama
alikuwa na akili timamu au la, wakati wa tukio hilo.
Amri hiyo ya Mahakama iliyotolewa na Jaji Samuel
Karua, ilitokana na maombi yaliyotolewa na Wakili Yusuph Shehe aliyekuwa
akiwatetea
Wakili Shehe alisema ameamua kutoa ombi hilo ili
kujiridhisha na utimamu wa akili za mshtakiwa kwanza kabla ya kuanza
usikilizwaji wa kesi hiyo kulingana na kumbukumbu za maelezo ya ushahidi
ulioko mahakamani.
Jana, kabla ya washtakiwa hao kuachiwa, Wakili wa
Serikali, Secy Mkonongo aliyekuwa akisaidiana na Clara Charles, alidai
kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali, kwa ajili
ya kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao.
Hata hivyo Wakili Shehe alidai kuwa mara ya mwisho
Mahakama hiyo iliamuru mshtakiwa wa kwanza, Rama, apelekwe katika
hospitali ya magonjwa ya akili kwa ajili ya uchunguzi wa akili yake.
Wakili Shehe alisema ripoti hiyo tayari
imeshawasilishwa mahakamani hapo kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Akili
Isanga tangu Juni 20, 2012, ikiwa imesainiwa na Dk Mndeme Erasmus na
kwamba inaeleza kwa mshtakiwa wakati akitenda kosa hilo hakuwa na akili
timamu.
No comments :
Post a Comment