PICHA KADHAA ZIKIONYESHA HALI ILIVYOKUA ARUSHA BAADA YA MLIPUKO KUTOKEA
Mlipuko Watokea Katikati ya Ibada na Kujeruhi Katika Kanisa Katoliki Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo akiteta jambo na mmojawapo wa viongozi wa Usalama - Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na
wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote
waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa.
Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika
eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa
tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa
Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu
kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya
waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao
wakiwa ni majeruhi.
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Ulinzi ukiwa umeimarishwa
Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa
habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi
mkali wa Polisi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Mh Gaundence Lyimo akielekea eneo la
tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana
na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri
wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
No comments :
Post a Comment