MWIGIZAJI Mahiri wa filamu Bongo Wema
Abraham Sepetu ndiye msanii anayelipwa fedha nyingi kuliko msanii
yoyote wa filamu katika kushiriki katika filamu kutoka kwa watayarishaji
wengine ili uweze kumshirikisha Wema Sepetu katika filamu yako kama
mwigizaji bila kujali anacheza scene ngapi gharama yake ni milioni kumi.
Wema ambaye kwa sasa anamiliki
kampuni yake ya utengenezaji wa filamu inayojuklikana kwa jina la
Endless Fame Film anasema kuwa moja ya sababu inayomfanya aweze kuchaji
gharama hiyo inajumuisha na kutumia kampuni yake pamoja yeye mwenyewe
kuigiza katika filamu hiyo, kwa hiyo ni wajibu wa mhusika kumudu gharama
hizo.
“Yaah kama mtayarishaji ananihitaji
kushiriki katika filamu yake atatakiwa kunilipa kiasi cha shilingi
milioni kumi kwa kushiriki katika filamu yake, lakini pia kuzingatia
ratiba ya utendaji usiingiliane na kazi zangu nyingine,”alisema Wema.
Inasemekana kuwa Wema ndio
msanii wa kike anayeuza filamu kuliko
mwigizaji wa filamu wa kike, pengine ndio sababu ya kuweza kutoza
gharama kubwa katika kushiriki filamu nje ya kampuni yake unapomuhitaji
Wema kwa ajili ya mapatano unaongea na mtendaji wake wa karibu Chiddy
Classic.
Gharama hizo ndio kubwa kwani hadi
sasa msanii ambaye amelipwa kwa kiwango cha juu ilikuwa ni milioni tano
ikiwa kama ndio kikomo cha malipo kwa wasanii wenye majina na wamiliki
wa makapuni yao, msanii kama Ray the Greatest hanunuliki kwani si rahisi
kushiriki nje ya kampuni yake ya RJ Company.
No comments :
Post a Comment