HabariMpasuko: ARUSHA HALI NI TETE MABOMU KILA KONA
HALI tete katika jijini la Arusha muda huu,Polisi wanapiga
mabomu ovyo,watu waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Soweto
wakisubiri kuaga miili ya watu waliofariki dunia katika shambulio la
kigaidi wametawanywa kwa mabomu.
Mbali na watu kutawanywa kwa mabomu hayo,Waziri Mkuu
aliyejiuzuru Edward Lawassa amenusurika kufa huku gari lake likiharibiwa
vibaya.
Polisi wameanza kupiga mabomu wakati wabunge wa CHADEMA walipoanza
kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake. Hali ni mbaya sana hata
watu wametelekeza magari na pikipiki zao, wabunge wote nao wamekimbia na
mbaya zaidi wanapiga mabomu kila mahali.
Hali ni tete, mabomu yanarindima sana hali ni tete magari ya mevunjwa
gari la Lissu laharibiwa, pikipiki zinavunjwa na polisi bila sababu.
Hali tete, tegemeeni msiba mwingine
Wametumia risasi za moto kupiga watu, gari la Tundu Lissu limevunjwa
vioo na jeshi la polisi. Wameumiza watu wengi sana! Hali ni mbaya sana!
No comments :
Post a Comment