KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA MAKETE ATUPWA JELA MIEZI 9 KWA KOSA LA KUTOTII AMRI YA POLISI
Mahakama
ya mwanzo Makete mjini wilayani Makete mkoani Njombe imemuhukumu katibu
wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya hiyo Bw Godfrey
Mahenge (63) kwenda jela miezi 9kwa kosa la kutotii amri halali ya
jeshi la polisi Makete
Akitoa
hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Makete mjini Mh. John
Mpitanjia amesema mtuhumiwa huyo alitumia lugha ya matusi kwa askari
polisi na kuwaita kuwa ni wauaji na kudai kuwa wametumwa na chama cha
mapinduzi (CCM)
Amesema
baada ya mahakama yake kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani
hapo na upande wa mashataka, mshtakiwa alitakiwa kutumikia kifungo cha
miaka miwili gerezani lakini kutokana na kutenda kosa hilo kwa mara ya
kwanza mahakama imeamua kumfunga miezi 9 gerezani ili iwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hiyo..
Mshtakiwa
huyo hakuwa na lolote la kijitetea na hakimu kumpatia adhabu hiyo na
kusema kuwa rufaa kwa mshtakiwa ipo wazi endapo anahisi ameonewa.
No comments :
Post a Comment