-
MAELFU WAMUAGA MPENDWA WAO….
-
AMANI NA UTULIVU VYATAWALA
-
WATU WAPUUZA TISHIO LA KUSHAMBULIWA, WAJITOKEZA KWA WINGI
Mkuu wa jimbo la Arusha magharibi na
Mchungaji wa kanisa la KKKT, Mch Kisiri amesema kuwa anasikitika kwa
Kifo cha Judith Moshi kilichokatizwa na watu/ mtu alie waita Wanyama na
Magaidi kwa kurusha Bomu katika mkutano wa CHADEMA.
Alisema kwamba Amani na utulivu tulionayo
ipo mashakani kutoweka kwa ajili ya viongozi wanaoshindwa kusoma Alama
za Nyakati huku wakiendeleza Porojo na Hadithi badala ya kujibu kero za
wananch, Badala yake kutumia Risasi na mabomu kuwatisha wananchi.
Katika ibada hiyo ya mazishi ya Marehemu
Judith Moshi aliwaambia watu waliojitokeza kwa wingi kanisani hapo
wasife Moyo wala kuogopa maana Mungu yupo upande wao.
Aidha aliwaasa polisi kuwa njia ya
kutumia risasi na mabomu kuwaua watu wanaodaiwa kuwa ni wakorofi sio
suluhisho kwani wakiuwawa hawa wengine watainuka.
REST IN PEACE MUNGU U NAWE DAIMAAA
ReplyDelete