Top News

Sunday, June 16, 2013

TAARIFA KUHUSU KUAHIRISHWA UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA HADI JUNI 30




Kufuatia tukio la mlipuko jana jumamosi Arusha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha chaguzi za madiwani katika kata zote nne (4) jijini arusha hadi jumapili ya tar 30/6/2013.



  • Uchaguzi wa Madiwani kata za Arusha Waahirishwa hadi Juni 30, 2013

Tume ya taifa ya Uchaguzi imesimamisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa udiwani ktk kata nne jijini Arusha. Akizungumza kwa njia ya simu na Radio TBC FM,kutoka Zanzibari mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi alisema kua wameamua kusimamisha uchaguzi huo ili kuwapa nafasi vyombo vya usalama kuchunguza swala hilo.

Alisema kua sheria inawapa mamlaka kufanya hivyo pale wanapogundua kuwa hakutakua na uhuru wa mpiga kura kwenda kupiga kura. Alisema haiwezekani uchaguzi ufanyike ktk hali kama hiyo huku kukiwa na wasiwasi.

Tume ya Uchaguzi Tanzania imeahirisha uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika leo hii katika kata 4 za Mkoa wa Arusha. Kata zingine 22 zitaendelea na uchaguzi kama kawaida. Hii inatokaana na mlipuko wa bomu wa hapo jana.Sasa utafanyika jumapili tarehe 30.6.2013

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ