Top News

Thursday, July 4, 2013

DR SLAA AMPONGEZA RAIS OBAMA

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amesema kwamba kitendo cha Rais wa Marekani Barack Obama kusema demokrasia siyo uchaguzi bali kuheshimu wapinzani kusikiliza watu na uhuru wa vyombo vya habari ni cha kupongezwa na ni ujumbe mzito kwa serikali ya CCM.

Dr Slaa amesema ujumbe huo wa Obama ni kwamba kiongozi huyo mkubwa anayeongoza Taifa kubwa duniani anaelewa kinachoendelea Tanzania.

Dr Slaa amesema ni wazi Marekani inaelewa kinachoendelea Tanzania kwamba ni pamoja na kupiga wapinzani, kusingizia wapinzani ugaidi na kufungia vyombo vya habari vinavyokosoa serikali.

Dr Slaa amesema kama kweli hii serikali ni sikivu basi iufanyie kazi kauli ya Rais Obama.``Hakika huu ni ujumbe mzito kwa serikali ya Kikwete`` amesema Dr Slaa.
  •  Obama aliyazungumza hayo baada ya kuulizwa kwa kile kinachotokea egypt

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ