Tanzania imekosolewa na gazeti maarufu la Marekani wakati Rais Obama akipokewa kwa nderemo na vifijo.
Gazeti hilo maarufu nchini Marekani la The New York Times, limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili yanayofanyika Tanzania.
Habari
hiyo iliyochapishwa katika toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la
kuteswa na kuumiza kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen
Ulimboka.
Mwandishi
wa habari hiyo amejaribu kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi
alivyotekwa na kuteswa kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.
Mwandishi
huyo amesema kuwa Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha
amani ndani ya ukanda wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
Kwamba
kutokana na sifa hizo, Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha
kutoka kwa mataifa mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo
mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.
Alisema
kuwa wakati Rais Obama akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za
binadamu na chama kikuu cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na
ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.
Ananukuu kuwa waandishi wamekuwa wakishambuliwa na
mmoja aliuawa akiwa anatekeleza kazi yake ya uandishi wa habari.
Aliongeza
kuwa Julai mwaka jana, serikali ililifungia gazeti huru la uchunguzi la
kila wiki la Mwanahalisi, ambalo lilikuwa likiandika kwa undani kuhusu
tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, ambalo lilihusisha uhalifu
huo na serikali ya Rais Kikwete.
Kamati
ya Kulinda Waandishi wa Habari yenye makao makuu yake New York nchini
Marekani, wiki jana ilimtaka Rais Obama kuliibua suala la uhuru wa
vyombo vya habari atakapokutana na Rais Kikwete jijini Dar es Salaam.
Gazeti hilo pia limetaja vurugu za kisiasa kuwa zilichukua sura mpya na
ambayo haikutegemewa wakati bomu la kurushwa kwa mkono lilipolipuliwa
katika mkutano wa
hadhara wa kampeni za uchaguzi wa madiwani wa
CHADEMA na kusababisha vifo vya watu wanne mkoani Arusha.
Source: New York times
http://nytimes.com/2013/07/01/world/...can-haven.html
No comments :
Post a Comment