Top News

Monday, July 1, 2013

VIDEO HIVI NDIVYO OBAMA ALIVYOTUA TANZANIA

Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili katika ardhi ya Tanzania muda huu katika ratiba yake ya mwisho wa ziara  barani Afrika.
Wadadisi na wachambuzi wa masuala ya Kiuchumi na kisiasa wanaeleza kuwa ziara ya Rais Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika.
Obama amewasili Tanzania baada ya ziara yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam.
Baadaye Rais Kikwete amemuongoza Rais Obama kuelekea Ikulu ya Tanzania kwa ajili ya shughuli zingine zilivyopangwa.
Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi
VIDEO

GONGA HAPA KUCHEKI VIDEO OBAMA ATUABONGO


No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ