Top News

Wednesday, July 31, 2013

Kama siku yako ya leo haijakaa poa Cheki hapa Kuifanya siku yako iwe poa....!

Jamaa fulani alikuwa na
tabia ya kujamba kwa
nguvu kila aamkapo
asubuhi. Mkewe alikerwa
sana na tabia hiyo,
alimkataza akachoka, siku
moja akamwonya kuwa iko
siku badala ya ushuzi,
utumbo utakuja kumtoka.
Jamaa alicheka sana
kusikia hilo. Siku moja
mke alilazimika kuamka
alfajiri awatengeze kuku
kwa ajili ya sherehe,
alipowatoa utumbo wale
kuku akakumbuka
alichowahi kumwambia
mumewe akaamua
kumtisha, akamnyatia
mumewe ambaye alikuwa
bado amelala na
kumuwekea utumbo
kwenye pajama lake na
kurudi jikoni. Muda si
mrefu mwanaume aliamka
akajamba kwa nguvu kama
kawaida yake, lakini
akahisi kitu cha baridi
ndani ya suruali, ile
kuvuta si akakuta utumbo.
Akapiga ukelele,’Mama
yangu nimekufa’. Mke
wake aliposikia akacheka
peke yake, akajua jamaa
kashaukuta ule utumbo.
Kimya cha kama nusu saa
kilipita. Hatimaye jamaa
akamfuata mkewe jikoni
akiwa amelowa jasho
pajama nzima.
JAMAA: Mke wangu yale
uliosema leo yametokea.
MKE: Yepi jamani?
JAMAA: Mke wangu
ulisema nikiendelea
kujamba utumbo utatoka,
leo utumbo si umetoka
kama ulivyosema
MKE: Pole mume wangu,
sasa?
JAMAA: Namshukuru
Mungu, nimejitahidi
nimeusindilia na vidole na
nimeweza kuurudisha
ndani wote.
MKE: Mungu wangu
umefanyaje?

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ