Top News

Tuesday, July 9, 2013

MAHAKAMA TABORA YAIRUKA KESI YA KILEO NA WENZAKE.

Henry Kileo Pamoja na wenzake wakielekea Mahakamani
Katika Hukumu ya dakika 7, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Tabora, imetoa uamuzi juu ya hoja za upande wa utetezi na kesi yenyewe, ambapo Hakimu Mkuu Mkazi kaamua kuwa, mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza mashtaka wanayoshtakiwa nayo Henry Kilewo na wenzake kwa madai kwamba Mahakamu Kuu Pekee ndiyo yenye uwezo wa kusikiliza kesi za Ugaidi.

Wamerudishwa gerezani Uyuwi.

Kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi wa CHADEMA nje ya mahakama ambapo akinamama walionekana wakiangua kilio huku wakilaani watu wanaotumia sheria vibaya kwa lengo la kuwatesa na kuwanyanyasa wapinzani wao kisiasa.

Itakumbukwa Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba amekuwa akizunguka kila kona na kijana anayeitwa Mussa Tesha huku akiwaaminisha Watanzania kwamba kijana huyo alimwagiwa Tindikali na CHADEMA na kusema atahakikisha CHADEMA wanalipa kwa kitendo hicho.

Jopo la wanasheria wa CHADEMA wanatarajiwa kutoa maamuzi katika muda mfupi ujao hatua zaidi za kuchukua na maelfu ya wafuasi wa CHADEMA kote nchini wameombwa kutulia.
Taarifa iliyotolewa mchana huu ni kwamba Jopo la Mawakili Nguli wa Chadema tayari wamewasilisha ombi Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora kuiomba mahakama hiyo kupitia upya uamuzi uliotolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora na Ikiwwzekana kuifutilia mbali kesi hii.

Ombi hilo limewasilishwa kwa Hati ya Dharura na Wakili Peter Kibatala ambaye aliwasilisha ombi hilo kwa niaba ya Jopo hilo la mawakili Nguli.

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ