Baada ya jana CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELO (CHADEMA) kushinda kwa Ushindi wa Kishindo ktk uchaguzi wa udiwani ktk kata nne za ELERAI, KIMANDOLU, THEMI na KALOLENI jijini Arusha hali iliyopelekea Wafuasi na Wapenzi wa Chama hichi Pendwa kusherekea hiyo jana,Mfuasi mmoja wa CDM ndugu GALLAS URASSA mkazi wa Sanawari Arusha, aliekua akiendesha pikipiki alifariki jana usiku mida ya saa 2 baada ya kugongana uso kwa uso na Gari aina ya Land Cruiser maeneo ya Sanawari juu karibu na kanisa la KKKT Loruvani.
Marehemu alikua akielekea nyumbani huku akishangilia ushindi huo. Inasemekana kuwa Marehemu Urassa alikua amekunywa pombe na wakati akiwa barabarani akielekea nyumbani kwake ndipo alipokutana na gari hilo liliokua ktk mwendo wa kasi na kumgonga. Marehemu alifariki pale pale na kuwa alikanyagwa na kupondwa kichwa!!
Mfuasi na Mpenzi huyu wa CDM ni mfanya biashara ya duka la Vifaa vya umeme sanawari pembezoni mwa bar ya SIMBA GRIL! Marehemu ameacha Mke mjamzito na watoto wadogo wawili.
BWANA AMETOA na BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, Amen!

Monday, July 15, 2013
MFUASI wa CHADEMA apoteza maisha wakati akishangilia Ushindii wa Udiwani Arusha!!
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment