Makubwa yameibuka baada ya msanii Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, kufungua kinywa
na kusema kuwa ugonjwa wake si bure bali amepigwa kipapai.
Akizungumza
na mwandishi wetu,Steve alisema kuwa kufuatia
kusumbuliwa na ugonjwa wa ajabu kwa kipindi kirefu sasa na madaktari
kushindwa kuelewa kila walipompima, staa huyo anaamini kuwa amerogwa na
msanii mwenzake.
“Nimetembea kwa wataalamu wa mambo ya asili na
kugundua hilo, sasa ninalazimika kuamini katika imani za kishirikina
ingawa ni kitu ambacho muda mrefu nilikuwa nikikipinga sana lakini kwa
hili ninaamini kweli nimechezewa na ndiyo maana niko hivi hadi sasa,”
alisema Steve bila ya kupepesa macho.
“Nashindwa kumtaja mhusika wa
tukio hili kwa sasa ila mwenyewe atakuwa anajua ni kwa kiasi gani
nimemgundua, nimejua kwamba wasanii hatupendani hata kidogo na wala
hakuna anayependa mafanikio ya mwingine.
“Ipo siku nitamtaja ila leo
ngoja niishie kusema kwamba nimechezewa na namshukuru Mungu kwa kuwa
hali yangu inaonesha matumaini ya kupona,” alisema Steve Nyerere.
Hivi karibuni, Steve alivimba mkono wake wa kulia, ilifika hatua alishindwa kulala na kutoka nje kutokana na maumivu.
No comments :
Post a Comment