Habari zenyu wapendwa, natumai mko vizuri kakitka kusaka shekeli, mi pia niko powa, na kwa wale ambao hawajisikii vizuri natumain mtajisikia powa soon
Ni hivi tangu nianze kuifahamu mitandao ya kijamii ni muda kidogo kiukweli nimebahatika kukutana na marafiki mbali mbali ambao sikuwahi hata kufikiri kama ipo siku ningekuja kuwafahamu, wapo ambao nilisoma nao na wengine tulipotezana miaka mingi lakini ndani ya mtandao kama Facebook nilikutana nawo na ilikuwa kama ni familia moja tena kukutana kiukweli inapendeza.
Sasa tangu nimeingia humu nimekuwa na marafiki wengi wa kike kwa wa kiume na wengine tunachat fresh tuu ila kuna watu humu kutokana na mtu anavyojipresent humu wanawish au wanakuwa na hamu ya kumuona huyu mtu ouyside fb or any bila kujali nini madhara yake.
Kwa mtazamo wangu finyu na kutokana na uzoefu nilioupata humu binafsi imetokea nikakutana nje ya FB na watu wawili ambao kabla sijakutana nao tulikuwa marafiki wazuri sana na tulikuwa tunachat sana ila baada tu ya kuamua kukutana nje ya FB na kujua ok kumbe Apex ndo huyu baaas ikawa ndo mwisho wa habari, hadi hapa nilipo mitamboni mawasiliano yamekatika kabisaaaaa.
Moral of the story (according to my thinking capacity) its better and good to remain anonymous here in FB and chat and be free with everyone, kuliko kutaka kuonana na kila unayezoeana naye humu urafiki unaisha na wengine ndo wanahama kabisa FB wakati mwanzo walikuwa wahudhuriaji/wachangiaji wazuri wa mada ambazo ulikua ukizi post.
Pia tabia hii imewafanya baadhi ya member humu jamvini kuja na Majina mpya kila leo kwasababu tuu huko nje ya FB au mitandao Mingine alishajitambulisha na akajulikana kama Apex sasa kutokana na watu wanavomjua huko nje anajikuta anashindwa kuchangia vitu flani flani au kuwa huru humu Mtandaoni. Binafsi sipendi tabia ya mtu kutumia Jina jipya kila, better be urself members!!
Kuna mtu leo kareport mtu na bosi wake wamekutana humu FB na kupanga kukutana ile kuonana kila mtu aibu na macho yakawatoka sasa anajiuliza aache kazi au la!! hiyo inaonesha kuwa ni moja ya side effect, licha ya kuwa na perception ya matarajio ya kukutana na bonge la mtu kumbe unakutana na mbilikimo si kuja kufedheheshana huku kama alivolalama retired sister.
Sasa mfano mie Apex tangu niingie FB or Twitter ID yangu ndo hii hii sijaibadili na wala sitaanzisha nyingine ili kumkwepa mtu au ili niulize au nichangie jambo flani, hii inanifanya niwe mgumu sana kukutana na watu nje ya JF as sitaki kuwa dormant maana hapa ndo kijiwe changu nikiwa idle or bored. Ukizingatia mitandaoni ndio mahali naweza punguza stess zangu au kupata ushauri kaza wa kaza. Kuna mtu mwingine anashindwa hata Kupost picha ya Mtu wake coz mtandaoni kuna tayari alie danganyana nae:
Mnisamehe wote ambao nitakuwa nimewakwaza kwa mitazamo yangu finyu ni mawazo yangu tuu na uzoefu wangu wa humu Mitandaoni
NOTE: If you prefer Apex as a friend, goodfriendship is here in FB outside there ni michosho na mastress tuu.



No comments :
Post a Comment