MAMA KANUMBA ADAIWA KUUZA MAGARI YOTE YA MAREHEMU MWANAE NA PESA KUNYWEA POMBE NA MAMA LULU!
Imebaki Hice tu ambayo nayo kesha pewa dalali atafute Mnunuzi. Ofisi nayo inapumulia mashine.
Xdeejayz yaibua mazito toka ndani ya familia hiyo.
Na Waandishi Wetu
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua Xdeejayz imeibua tuhuma nzito toka
kwa familia ya Marehemu Stiven Kanumba inayomtuhumua Mama wa msanii
Flora Mutegoha kuuza mali za mwanae kisha pesa kunywea pombe na mzazi
mwenzake Mama Lulu huku akiisahau familia.
Habari za uhakika toka
ndani ya familia hiyo zilisema kuwa Mama Kanumba hivi karibuni alianza
kuiuza gari ya kifahali ya V8 na alimuuzia shilingi milioni 30 Mama
Salma Mtambo ambae ni mfanyabiashara maarufa Jijini Dar kisha pesaa hiyo
kwenda kunywea pombe yote na kuisahau familia yake.
Aidha chanzo
hicho kiliendelea kusema “ Haikupita muda tena ameuza gari nyingine aina
ya Mark II kwa shilingi milioni 6 kisha kula bata pesa yote na sasa
hivi ameshawapa madalali kazi ya kumtafuta mteja wa kuimalizi Hice
aliyokuwa anaitumia marehemu kwa ajili ya kazi zake za Location” Alisema
dada huyo ambae ni ndugu na Mama Kanumba na aliomba hifadhi ya jina
lake kwa usalama wake.
Habari zaidi ziliendelea kusema kuwa tangu mama Kanumba ashinde kesi ya
mirathi hiyo ya mwanae amekuwa hana ushirikiano mzuri na baadhi ya ndugu zake “ Yani kweli pesa inabadilisha mtu huyu mama sisi ni ndugu yetu kabisa lakini tangu azitwae mali za mwanae basi hataki ushirikiano
wowote na sisi kwa mfano zile pesa za rambirambi ya msiba milioni sabini
akachukua milioni 50 akanunua nyumba maeneo ya Mbezi Temboni hilo
tulimpongeza” Alisema bint huyo mdogo
Msichana huyo aliongeza kusema “ Lakini baada ya hapo mama huyu alikutana na Mama Lulu ambapo hali
imekuwa mbaya ambapo wenyewe wameshauriana nini sijuia na walianza
kuiuza ile V8 ambapo pesa yote walilia bata hadi ikaisha na hivi
karibuni akaiuza gari nyingine ya marehemu aina ya Mark II na pesa hiyo
wameitafuna yote hadi imeisha na sasa hivi anaimalizia ile Hice ambayo
ndio ilikuwa tegemeo kwa ajili ya kampuni sijui tufanyaje jamani?”
Alimaiza kusema bint huyo kwa uchungu.
Xdeejayz baada ya kupata taarifa hizo lilijaza mafuta gari ya ofisi na
kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mama huyo kwa ajili ya mahojiano
na kufanikiwa kufika nyumbani kwa Mama Kanumba ambapo waandishi wetu
wakiwa kamiri na kamera za siri aina ya Kalamu ambapo waligonga geti
hilo jeusi na kufunguliwa na msichana ambae alijaitambulisha kwa jina la
Husna ambae alisema kuwa yeye ni house girl na mara baada wanahabari
wetu kijitambulisha na kuomba kuongea na Mama Kanumba msichana huyo
alijibu kuwa Mama huyo alikuwa ametoka hivyo labda waandishi wetu warudi
tena kesho yake au baadae.
No comments :
Post a Comment