MIEZI nane baada ya
kufariki dunia mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’, hatimaye mume wa pili wa staa wa
filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Ahmed Kushi ameibuka na kudai kwamba
anatambua kwamba staa huyo bado ni mkewe na anat aka ampatie mwanaye aliyezaa
naye.
Kwa muda mrefu
kulikuwa na taarifa kuwa Wastara aliachana na mwanaume huyo kwa talaka kabla ya
kuolewa na Sajuki lakini kuibuka kwake na madai kuwa bado mwanadada huyo ni
mkewe kumezua mshangao mkubwa.
Akizungumza hivi
karibuni,Kushi alifunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye na Wastara walifunga
ndoa ya Kiislamu mwaka 2000 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye
Fares.
Alisema: “Kisheria
bado ni mke wangu kwa kuwa nilikuwa nimempa talaka moja tu wala hazikufika
tatu,” alisema Kushi na kudai kwamba ndoa yake na staa huyo ilidumu kwa mwaka
mmoja na nusu na kuvunjika kutokana na kutawaliwa na migororo.
Jamaa huyo alidai
kuwa zaidi ya mara tatu amekuwa akimtaka Wastara ampatie mwanaye huyo ambaye
kwa sasa ametimiza miaka minane bila ya mafanikio.
Kushi alipobanwa na
kumuulizwa kwa nini ameibuka wakati huu baada ya Sajuki kufa na mbona
hakujitokeza kwa zaidi ya kipindi cha miaka kumi iliyopita? Pia akaulizwa kwa
nini ameamua kutafuta umaarufu kwa kumdhalilisha? Akaishia kukaa kimya.
Baada ya Kushi
kuibuka na ishu hiyo yenye utata, gazeti hili lilizungumza na Wastara ambapo
alikuwa na haya ya kusema:
“Kuhusu mtoto, kama
kweli alikuwa na lengo la kumchukua mwanaye na ananijua, basi atakuwa anawajua
wazazi wangu hivyo angefuata utaratibu.
“Hakuna utaratibu
kama huo kama kweli anamhitaji mwanaye angeenda kwa wazazi wangu, huko ni
kunidhalilisha kwa kuwa ananiona mnyonge baada ya kufiwa na mume wangu Sajuki.
“Kama siyo
kunidhalilisha ni nini? Naomba asitumie jina langu kutafuta umaarufu kwa
kunichafua. Naomba aache kwa sababu ananiongezea maumivu juu ya maumivu.”
Kuhusu madai kwamba
bado ni mkewe, Wastara alilia: “Hivi huyo mtu alikuwa wapi muda wote nikiwa na
Sajuki? Mbona hakuibuka wakati mume wangu akiwa hai? Najua anatumia kigezo cha
kuondoka Sajuki kunionea lakini Mungu anajua.”
Pamoja na
kumbembeleza aeleze kama kweli aliwahi kufunga ndoa na Kushi, Wastara alisema:
“Sitaki kumzungumzia mtu, naomba watu wawe na huruma kwangu, wasitumie kigezo
cha kumpoteza Sajuki kunidhalilisha.”
Alitafutwa shehe wa
Msikiti wa Nuur wa Magomeni-Mapipa jijini Dar, Juma Simba ili kupata ufafanuzi
juu ya talaka moja ambapo alimpinga Kushi kwa kusema kuwa kisheria Wastara si
mkewe tena.
“Kumpa talaka moja si
sababu ya kuendelea kuwa mke wake mpaka leo hii, sheria inasema kuwa Kushi
alitakiwa kumrejea Wastara kabla ya miezi mitatu kupita tangu alipompa talaka
moja,” alisema na kusisitiza kuwa ndoa hiyo ilishakufa.
Awali ilidaiwa kuwa
Wastara aliwahi kuolewa mara mbili kabla ya kufunga ndoa na staa mwenzake wa
filamu, Sajuki.
Ndoa ya kwanza ya
Wastara aliifunga mwaka 1998 na Juma Mpemba ambaye alibahatika kupata naye
mtoto mmoja wa kiume aitwaye Samir.
Sajuki alikuwa mume
wa tatu kwa Wastara ambaye naye alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye
Farheen.
via-GPL
No comments :
Post a Comment