Top News

Thursday, August 1, 2013

Padri, Nitasamehewa kwa hilo, Kama siku Yako haijakaa powa unaweza ukacheki hapa kuiweka powa.

Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha,
kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja
akaingia,
akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara
ya
msalaba akaanza kuungama.
== "Padri naungama dhambi zangu, leo
nimefanya
dhambi kubwa sana"
"Endelea...."
...
...
== "Bosi wangu aliniita nyumbani kwake
akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni
50,
akasema nisipotoa maelezo ya kutosha
atanipeleka
polisi.
Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa na pesa
kweli
niliiba, nikatazama huku na huku nikagundua
tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola
nikamuua.
Nitasamehewa?"
"Utasamehewa...!! " == "Basi wakati nataka
kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi...!!
Akaniuliza nimemfanya nini mume wake.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili
peke yetu, nikamuua na yeye. Nitasamehewa na
hiyo?" "Utasamehewa... "
== "Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke
lakinimlinzi akakataa kufungua geti akasema
amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea
kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua
tuko
wawili peke yetu nikamuua. Nitasamehewa?"
"Mmm!! Utasamehewa... ."
== "Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto
wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani
tena.
Akasema amerudi nyumbani na kukuta
yalotokea,
lakini akanionyesha diary ya baba yake
inayoonesha
kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa.
Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema
ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili
peke yetu nikamuua. Diary nikaichomamoto.
Nitasamehewa na hilo?"
Kimya........ "Padri, Nitasamehewa kwa hilo?"
Kimya.........
Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo.
Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou
za
mapadri kama linatikisika.
Kufungua akamuona Padri kajificha katikati ya
majoho anatetemeka.... .
"Sasa baba mbona umenikimbia?"
Padri kwa taabu akajibu...
"Nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko
wawili peke yetu........"

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ