Sunday, May 18, 2025

Sunday, August 11, 2013

Taarifa ya kilichojiri Morogoro kuhusu Sheikh Ponda

Ifuatayo ni habari moja yenye muunganisho wa taarifa mbili kumhusu Sheikh Ponda. Awali ni taarifa ya yaliyotukia Morogoro hapo jana na inayofuata ni habari ya juzi kuhusu agizo la DPP la kutaka akamatwe.
KATIBU wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda, alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumizwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi kwenye bega lake la kulia wakati akiekelea katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya kumalizika kwa kongamano ya Dini ya Kiislamu.
Mkasa huyo ulitokea Jumamosi Augosti 10, mwaka huu majira ya saa 12:15 za jioni eneo la barabara ya Tumbaku karibu na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba, Manispaa ya Morogoro.
Shekhe  Ponda alishiriki katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo.
 Kongamano hilo lilipata baraka zote na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, ambalo lilitoa  masharti kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni kutokashifu dini nyingine wala viongozi wa serikali.
 Sakata la kutaka kutiwa mbaroni kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa kukiuka masharti ya Mahakama aliyopewa baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje wa  kutakiwa asitende kosa lolote la jinai anapotumikia adhabu hiyo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai kuwa Shekhe Ponda
baada ya kutoka ndani ya gari eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita chache katika barabara ya Tumbaku alitelemka na wakat akitaka kuingia garini ilifayuliwa risasi iliyompiga begani.
 Ustaadh Msema alidai kuwa baada ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa wameambatana naye walimchukua na kumpakiza kwenye Pikipiki hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupoatiwa matibabu.
 Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika hospitali, waliona anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo walipoamua kumwondoa na kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja.
Akizungumzia kwa kina hali ya Shekhe Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu hai licha ya kuumia vibaya begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo jingine hususani Jijini Dar es Salaam kupata matibabu zaidi.
Alisema viongozi wa Umoja huo hauwezi kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu ambapo kumekuwa na sinto fahamu.
Baadhi ya walinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe Ponda aliletwa hapo kwa usafiri wa Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia getini.
Walisema walimwingiza adi mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa na watu ambapo muda si mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini hapo.
 Hata hivyo walinzi hao walisema, baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda waliamua kumyanyua na kumbeba mabegani na kutoka naye mlango mwingine wakimlazimisha mlinzi kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa usafiri wa Pikipiki kusikojulikana.
Kufikishwa kwa Sheshe Ponda katika Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na Mwenyekiti huyo ambaye alidai  kuwa waliamua kumwondoa baada ya kuchekewa  kupatiwa huduma.
Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na Polisi na kufariki dunia. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilongine akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea kwa tukio hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo cha Shekhe Ponda.
 “ Nimepingiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia , ujumbe umesambazwa kwenye simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna kifo wala maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili” alisema Kamanda huyo.
Juhudi za kufuatilia sakata la uvumi kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa kazi na Ripota a wetu huyu na usiku wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe Ponda yu hai isipokuwa ameumia vibaya sehemu ya bega .
 “ Nipo katika eneo ambalo Shekhe Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo hatuwezi kupataja kiusalama , isipo kuwa ameumia vibaya kwenye bega lake. Lakini yu hai wala hajafa” alisema Msema.
Polisi Mkoani hapa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo, nasi twaendelea kufuatulia kwa ukaribu.
----------------------- MWISHO wa Taarifa kutoka kwa John Nditi -----------------------
AGIZO LA DPP LILILOCHAPISHWA KWENYE HABARI KATIKA GAZETI LA DAILY NEWS SIKU YA IJUMAA, AGOSTI 9, 2013
Gazeti la Daily News (Tanzania) siku ya Ijumaa tarehe 9 Agosti 2013 (habari nzima imenukuliwa hapo chini) lilikuwa na taarifa inayosema kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka wa Tanzania, Dk Eliezer Feleshi, ameitaka polisi kumkamata Sheikh Ponda Issa Ponda kwa kuvunja amri ya mahakama ya kutojihusha na matukio ya uchochezi.
"Alitiwa hatiani kwa kosa hilo hilo, lakini alikuwa bado anafanya mambo yanayohatarisha usalama wa nchi," alisema Feleshi. "Tunatarajia polisi watatumia nguvu zao kwa busara kumkamata Sheikh Ponda na kumpeleka mahakamani kwa hatua za kisheria."
Ponda alikamatwa mwezi Oktoba kwa kuchochea vurugu uliopelekea kuharibiwa kwa mali jijini Dar es Salaam na alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela. Aliachiwa kutoka jela mwezi Mei baada ya Hakimu wa Wilaya, Victoria Nongwa, kuifuta hukumu ya jela, kwani tayari Ponda alishatumikia miezi saba akiwa kwenye mikono ya polisi.
Polisi visiwani Zanzibar wanamfuatilia Ponda kwa sasa baada ya ripoti kwamba ameitisha maandamano dhidi ya serikali. Ponda, ambaye ni katibu mkuu wa Baraza la Jumuiya za Kiislamu, anatuhumiwa kuwaambia wafuasi wake kupigania haki zao.
"Hii haiwezekani. Hatuwezi kumuacha mtu akiuke amri za mahakama na kutokuadhibiwa," alisema Feleshi. Polisi wamewakamata na kuwahoji watu watano wanaoshukiwa kumhifadhi ulamaa huyo.
    THE Director of Public Prosecutions (DPP), Dr Eliezer Feleshi, has called for the arrest of the Secretary of the Council of Islamic Organisation, Sheikh Ponda Issa Ponda, for disobeying a lawful court order.
    Sheikh Ponda was in May, convicted of forcible entry into a plot by the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam. He was given a oneyear suspended jail term and directed to refrain from taking part in incitement activities likely to lead to breach of the peace in the country.
    Dr Feleshi noted that recent reports have it that the cleric is engaged in organising religious gatherings in Zanzibar, which threatened peace in the Isles. "Such a behaviour is intolerable," the DPP said in an interview with the 'Daily News' on Wednesday.
    He added: "We hope the police will exercise their powers wisely to arrest Sheikh Ponda and take him to court for penal actions." Dr Feleshi said what Sheikh Ponda was currently doing was contrary to his sentence. "He was convicted of a similar offence, but was still conducting acts that threaten the public order and concord.
    This is not acceptable. We cannot let one disobey court orders and go on unpunished," he said. Counsel for Sheikh Ponda Juma Nassoro was not reached for comment on the matter.
    Reports from Zanzibar have it that police are tracing Sheikh Ponda's whereabouts. He is alleged to have called on the citizens to initiate strikes against the government. Zanzibar Commissioner of Police, Mussa Ali Mussa was reported to have said that Ponda's statements breached police directives to religious leaders to avoid giving messages which threaten the country's peace.
    The police in the Isles arrested five persons who reportedly gave shelter to the controversial Muslim Sheikh. They were interrogated for hosting Ponda.
    Sheikh Ponda, according to the police, had requested the believers to be ready to fight for their rights and stressed that they should soldier on.
    Adjourning the Zanzibar House of Reps budget session for 2013/2014, the Second Vice-President, Amb. Seif Ali Iddi announced a ban for Sheikh Ponda to set his foot in the Isles for the purpose of inciting the people. Amb. Iddi warned that the government should not be blamed for serious measures that would take against leaders of such calibre.

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ