Top News

Thursday, August 15, 2013

Ujuzi: Fahamu Jinsi Ya kununua Bidhaa kupitia Internet (PayPal)

Katika matumizi ya internet kumekuwa na huduma mbalimbali kwenye websites za uuzaji wa bidhaa na kutoa huduma (mfano: amazon, ebay, ebooks e.t.c) ambazo zinahitaji malipo ya bidhaa hizo yafanywe kupitia PayPal account. Na huu ni msaada wa kujuwa zaidi kuhusu hii PayPal, na maelezo haya yatalega kufahamu yafuatayo:
  • PayPal ni nini?
  • Inafanyaje kazi/ inatumikaje?
  • Faida zake
  • Jinsi ya kujiunga na requirements za kujiunga
  • Na kwa kuwa huduma hii inainvolve money transactions, je inausalama kiasi gani?
Pia kuna maelezo mengine ya ziada nje ya hizo guidelines ambayo yatakuongezea ujuzi .

 Ok paypal kwa uelewa wangu ni mfumo wa malipo ambao inabidi ujisajili baada ya kuwa na kadi yako ya aidha VISA, Mastercard n.k

Mfano nilinunua kadi kupitia BankABC kwa $20 ambayo baada ya kununua unaachana na makato mengine yote hadi inapo expire.

Labda kama utakwenda kutoa fedha kwenye ATM utachajiwa Tshs 500.00 kama transcation charge.

Baada ya hapo nikaisajili paypal.

Kwa hiyo paypal ni nini sasa?

Paypal ni kama nilivyosema ni mfumo ambao mtumiaji anabidi ajisali ili aweze kulipia vitu online. Na siyo kulipia tu hata kupokea.

Mfumo huo unamuhakikishia mtumiaji usalama wa matapeli au hackers. Mfumo huo hautoi details za akaunti yako kwa mnunuaji na hivyo kuepuka madhara yasiyo ya msingi.

Pia mtandao huu kama una compromise na mnunuaji wanaweza kukurudishia hela kama hutapata bidhaa yako.

Lakini ili uweze kuisajili kadi yako inabidi uende kwenye mtandao wao ambao ni www.paypal.com na kujaza details za kadi yako kisha utakuwa unverified member.

Itabidi ulink card yako kwa kui conferm. Hapo ukifanya hivyo watapeleka namba kwenye bank yako na itakubidi urudi kwenye tawi ulilofungulia ili upate namba hiyo na kuja kuijaza na kuwa verified.

Wanafanya hivyo siyo kwa usumbufu bali makusudi maana mtu anaweza akaiba au akaiokota na kuisajili kisha akafanya malipo online kadi ina credit balance. Kwa hiyo namba inapelekwa kwenye tawi ili kama siyo yako watakutambua kuwa siyo yako na hutapewa namba hizo.

Mara ukiwa verified unaweza kununua vitu online kwa salama na haraka.

Mfano umeona kitu mtandao wa ebay ambao basi unaenda buy now na kisha utatakiwa kulipa kama muuzaji ana support paypal.

Once ukiconferm ni hapo hapo hela yako inakatwa kwenda kwa muuzaji na kisha wanakujulisha kuwa umekatwa kiasi fulani kwa ajili ya kitu ulichokinunua. Charges anakatwa muuzaji wa bidhaa na siyo wewe. Hapo unaepuka mlolongo wa kwenda mabank kama NBC, CRDB n.k kisha kuwa charged hela nyingi kwa ajili ya kutuma fedha hiyo.
Ni nzuri na salama kaka.

Kuna maswali kama
  • Je ni bank gani zinazo-support matumizi hayo ya paypal?
CRDB, NBC kuna na BARCLAYS nk.
  •  Je ili kujiregister paypal ninatkiwa kuwa na kiasi gani cha fedha kama minimum requirement kwenye account yangu?
 Balance ya chini ni ile dhamana ya bank ambayo ni U$20 unaweza kuijisajili.
  • Payments nyingi za paypal zinatumia currency ya USD ($) na huku kwenye bank account yangu nimedeposit TZS je hio currency exchange inafanywa na nani, paypal au ni bank yangu inaconvert na kuwalipa paypal in USD?   
Currency yoyote haina shida ila mimi nilichagua dola kwa sababu najua exchange rate nyingi za mabank zipo juu kidogo tofauti na za mtaani. Kwa hiyo kama nataka kununua kitu online nanunua dola mtaani naenda kudeposit kisha nanunua nikitakacho.

4 comments :

Designed By ApexbnewZ