HUKU
kukiwa na madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui amekamatwa na
kufungwa nchini Brazil kwa kunaswa na unga, mwanadada huyo ameibuka na
kufafanua juu ya tuhuma hizo.

Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya
simu kutokea Brazil, Aisha alisema ameshangazwa na madai hayo wakati
yeye yuko nchini humo akiwa amemfuata mchumba wake ambaye jina lake
hakuwa tayari kulianika.
“Jamani hayo madai ya kwamba nimefungwa huku kwa kesi ya madawa ya kulevya mimi mwenyewe nayashangaa. Niko huku kwa mwezi wa nne sasa, nimekuja kwa mchumba wangu. Hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu

“Wakati
naondoka Tanzania ilikuwa kimyakimya kwa kuwa nilijua kuna baadhi ya
watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichokifanya.
“Naomba
Watanzania wajue niko huru kabisa, naendelea na shughuli zangu kama
kawaida. Natarajia kurudi Bongo hivi karibuni,” alisema Aisha.
No comments :
Post a Comment