Baby Madaha afungua njia kwa wanao mtaka kimapenzi
Leo katika interview na baby Madaha ambaye hivi karibuni
amesaini mkataba mnono na kampuni ya Candy n’ Candy Records ya
jijini Nairobi nchini Kenya , Bongomovie.com wameweza kupata mambo matano
ambayo mashabiki wa mwanadada huyu watakuwa hawajui kumhusu yeye. Katika interview hiyo, baby Madaha ametaja mambo matano ambayo anasema
mashabiki wake wanahitaji kuyafahamu kumhusu yeye. Mambo hayo ni haya
yafuatayo: 1. I’m single ( Sina mpenzi) Mwanadada
huyu amesema kuwa kwa sasa yupo single na yuko bize na PESA. Ila
kama kuna mwanaume mwenye nia ya dhati anaweza kumtafuta. 2. Anasoma degree ya sanaa kwenye sayansi ya siasa na historia
(B.A- Political science and History) - chuo kikuu huria jijini Dar
es Salaam.. 3. Mama yake mzazi ndio rafiki yake mkubwa maishani 4. Ni mpenzi wa soka na ni mshabiki wa Chelsea na anavutiwa na
Kevin-Prince Boateng wa club Schalke 04 ambaye ndiye alisababisha
akanyoa nywele staili aliyonayo baby madaha kwa sasa.
No comments :
Post a Comment