Top News

Monday, September 30, 2013

Gazeti la Mwananchi laendelea kupiga kazi Kama kawa.

Kama ingekuwa miaka 10 iliyopita, waandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi wangechukua likizo ya siku 14 kwenda kusalimia ndugu jamaa na marafiki wakati wakisubiri serikali iwaruhusu tena kuendelea kuchapisha magazeti yao baada ya kufunginiwa.
Gazeti
Lakini mambo yamebadilika. Licha ya serikali kulifungia gazeti la Mwananchi kwa siku 14 kwa kile ilichodai kuandika habari za uchochezi, wasomaji wanaweza kuendelea kusoma habari zake. Asante kwa internet iliyowezesha hili kufanikiwa.
Gazeti hilo limeendelea kuandika habari, kama vile hakuna kilichotokea kwa kuziweka kwenye website yake ambapo mtu yeyote mwenye internet anaweza kuendelea kusoma habari zake.
Serikali iliyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013 kutokana na kile ilichosema ni ‘mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.’
Gazeti la MWANANCHI lilifungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013. Adhabu hiyo ilitangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 Septemba,2013.

Nalo gazeti la MTANZANIA lilifungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi. Taarifa ya serikali ilisema gazeti hilo limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari.
-Bongo5

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ