
Na Luqman Maloto
BINAFSI
nafahamu kwamba Irene Uwoya aliwahi kuwa staa mkubwa nchini lakini
akafanya makosa na sasa ameshuka chati. Ameporomoka kwa kiasi kikubwa
sana.

Elizabeth
Michael ‘Lulu’, baada ya ‘ajali’ yake na marehemu Steven Kanumba,
alikaa mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini baada ya kutoka
ameonekana kuwa na mafanikio makubwa kuliko Uwoya ambaye siku zote yupo
mtaani.
Pengine
kuna aina fulani ya maisha ambayo Uwoya amejichagulia maana akina Rose
Ndauka, Aunt Ezekiel, Wema Sepetu na wengineo wamekuwa wakifanya vizuri,
wanamfunika sana. Ameshindwa kujisahihisha, ataendelea kusugua.
Najua
kwamba Uwoya ana hali mbaya kisanii, amechoka, muonekano wake
hausisimui tena, amepoteza mashabiki, kwa maana hiyo hauzi. Dili za
kucheza filamu zinaota mbawa kila kukicha, maprodyuza wanataka wakali
ambao wanafanya biashara sokoni.
Naelewa
kuwa hivi sasa katika ulimwengu wa masupastaa, Uwoya amebaki
msindikizaji lakini sikuwahi kufikiri kwamba anaweza kufikia hatua mbaya
kiasi hicho. Kafikishwa mbaroni kwa wizi wa simu? Yaani wizi wa simu ya
mkononi! Anatia huruma.
Yamemfika
yapi? Sitaki kuamini kama Uwoya anashindwa kununua simu halali. Akili
nyingine inaniambia kuwa hawa dada zetu wanaharibiwa na uchu wa kupenda
vitu vya juu lakini uwezo ni mdogo. Je, huo wizi wenyewe alifanyaje?
Atakapofikishwa
mahakamani pengine itajulikana kama kweli amehusika na wizi huo, basi
itafahamika ameufanyaje. Ni yeye moja kwa moja au kupitia kwa mtu
mwingine? Dunia ina mengi, ni vizuri hili jambo likafika kortini, huko
tutajua ukweli halisi.
Swali
langu ni hili, kama kweli ile simu alinunua kwa nini pale kituoni
hakutoa risiti? Hata kama ingekuwa nyumbani, alishindwa nini kuagiza
aletewe kuthibitisha kama ni mali yake? Maswali hayo mawili yanaongeza
uzani kwenye madai kwamba ile simu ni ya wizi.
Ni
ya wizi sawa, je, ni kweli Uwoya anaweza kuiba simu? Inawezekana kabisa
akatega Kariakoo halafu amvizie mtu na kumchomolea? Maana mashtaka
dhidi yake ni Wizi wa Maungoni, yaani wizi wa kumchomolea mtu kitu
kutoka mwilini.
Kesi
ipo Msimbazi Polisi na imeandikwa kwenye kitabu cha ripoti za
kumbukumbu (report book ‘RB’) kwa nambari MS/RB/8522/2013. Hata hivyo,
simu yenyewe iliyoibwa ina thamani kubwa, nahisi Uwoya aliinunua kwa mtu
ambaye ndiye mwizi.
Mikono
ya Uwoya na vidole vyake vilivyo, haoneshi kama anaweza kuwa mkali wa
kuchomolea watu. Hata kama kaishiwa na kupigika, siyo rahisi akafanya
hivyo. Sura yake haioneshi ushujaa wa ‘kupiga ndole’ lakini ya Mungu
mengi.
Labda
kauziwa lakini yeye ndiye kakutwa na mali ya wizi (aliyekutwa na ngozi
ndiye aliyeiba ng’ombe). Kama ipo hivyo, hilo nalo ni tatizo kubwa.
Maana yake yeye naye ni mmoja wa watu wanaowafanya wezi waendelee
kufanya uporaji. Anawafadhili kwa mlango wa nyuma.
Tusimamie
hapa kwamba kama alinunua, basi Uwoya ni mfadhili wa wezi kwa sababu
mtu anayenunua mali ya wizi, anawasaidia wezi kuendelea kuishi kwa
uporaji. Kwa maana hiyo siyo mtu mzuri, hafai kwenye jamii.
Kwa
mwenendo huo, naamini ndiyo maana ameporomoka, anakosa sifa ya kuitwa
kioo cha jamii. Inawezekanaje awe mfano wa kuigwa ikiwa yeye ni kirusi
katika hiyohiyo jamii? Mtu unajua kabisa hii mali ya wizi unainunua kwa
bei chee halafu unaona raha.
Kununua
mali ya wizi ni hujuma nzito, ni ukosefu wa huruma kwa sababu wakati
wewe unauziwa mali hizo kwa bei nafuu sawa na bure, halafu unaitumia kwa
nafasi huku ukijionesha, mwenzako anateseka mno.
Fikiria
kama wewe umejibana, ukajitutumua kununua simu aina ya iPhone 5 kwa
shilingi milioni 1.6. Umeitumia wiki mbili tu unaibiwa, halafu mtu
mwingine anakuja kuuziwa kwa shilingi 400,000 au 300,000. Itakuuma
kiasi gani?
Bila
shaka utamchukia mwizi na yule aliyeuziwa, kwani angekuwa muungwana
asingekubali kununua. Laiti angekuwa raia mwema, angesaidia huyo muuzaji
akamatwe ili aliyeibiwa arudishiwe mali yake. Kutumia mali ya wizi ni
dhuluma, ni wizi.
Uwoya
alikamatwa na simu ya wizi aina ya iPhone 5, kwa hiyo kama aliuziwa, na
kwa mujibu wa tafsiri ambayo nimeielezea hapo juu ni wazi kwamba yeye
siyo raia mwema. Ukweli uzidi kusimama kwamba hafai kuitwa kioo cha
jamii.
Je,
ni tamaa ya kutaka vitu vizuri wakati pesa hana? Ajioneshe mjini kwamba
anamiliki iPhone 5 kumbe ni ya wizi, ameipata kimagumashi. Namshauri
Uwoya aache mtindo wa kuishi kimagumashi, kama hana akubali hali halisi.
Si kulazimisha maisha ya gharama, matokeo yake ndiyo haya.
ANGEMTII MUMEWE YASINGEMFIKA HAYA
Nikiongoza
jopo la waandishi kutoka Global Publishers Ltd, mwaka jana,
tulifanikisha kumsuluhisha Uwoya na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’
kutokana na mgogoro wa nguvu ambao ulikuwa unaitikisa ndoa yao.
Malalamiko
ya Kataut yalijikita katika uaminifu, kwamba Uwoya alikuwa anaonesha
alama nyingi kuwa si mwaminifu kwenye ndoa yao. Mume huyo, alisema
kwamba amenunua vifaa na kuanzisha kampuni ili mkewe ajisimamie katika
kazi zake za filamu lakini mke hataki.
“Analipwa
pesa kidogo ambayo akifanya shopping tu zinakwisha, maprodyuza wanapata
fedha nyingi, yeye anafanya kazi, anauza sura tu lakini pesa hakuna.
Nataka atengeneze filamu zake ili apate pesa za kuonekana lakini haelewi
wakati kila kitu nimeshanunua,” Kataut alilalamika.
Kataut
alikuwa na nia ya dhati kabisa ya kumwokoa Uwoya na pengine kama
angefuata mwongozo wa mumewe leo hii asingeporomoka kama alivyo. Pengine
yanayomkuta leo ni malipo ya kile ambacho alimtendea mwanamme huyo.
Mke
wa mtu kunaswa hotelini na kijana wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’, ni aibu sana! Kabla ya hapo zilishaibuka stori kwamba
amegombana na supastaa Jacqueline Wolper kisa mwanaume. Alimtesa sana
Kataut wa watu.
Akiwa
yupo ndani ya ndoa, akaingia kwenye mgogoro na boyfriend wake wa
zamani, Hamis Ramadhan Baba ‘H-Baba’, akadai eti katika wanaume wake
wote waliopita, ambaye hawezi kurudiana naye ni H-Baba. Huyu ni mke wa
mtu.
Tafsiri;
kumbe pamoja na kuwa kwenye ndoa, anaweza kurudiana na wanaume wake
wote waliotangulia isipokuwa tu H-Baba. Je, unamuonaje huyo? Ni mke wa
mtu kweli?
Mke
wa H-Baba, Flora Mvungi naye akamvaa Uwoya, akamchamba, wakachambana.
Mke wa mtu anagombana na mwanamke mwingine kisa mwanaume tofauti na
mumewe. Ninaposema hafai kwenye jamii namaanisha kweli.
Matukio
ambayo anakumbana nayo hususan hili la wizi wa simu, achukue kama
changamoto na ajisahihishe pale alipojikwaa. Amwangukie mumewe pengine
mambo yakamnyookea. Iwe kama ameiba yeye moja kwa moja au aliuziwa,
ajisahihishe.
Source:Global Publishers

No comments :
Post a Comment