Top News

Monday, September 23, 2013

Mwanamke wa Kizungu ahisiwa kuongoza shambulio la kigaidi nchini Kenya

Mwanamke raia wa Uingereza, Samantha
Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa* kuongoza kundi la magaidi wa
Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya Westgate ya jijini Nairobi
nchini Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68 na kujeruhi wengine zaidi
ya 175.


Tayari mashirika makubwa ya
habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes yameandika habari
kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa magaidi hao
walioshambulia Westgate.

Nayo akaunti ya Twitter ya
American Jihad Watch ‏@watcherone, imepost picha ya gaidi wa kike
iliyedai ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na kudai kuwa
‘huenda’ akawa ni The White Widow. “Female jihadi caught on mall camera
at Westgate Centre Shopping mall

earlier yesterday may be infamous

‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.


Picha ya gaidi akiwa ndani mall hiyo

Kwa mujibu wa baadhi ya watu waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa kizungu.

Kwa mujibu wa CNN, magaidi
watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya, Uingereza, Finland na wawili wa
Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.

Hata hivyo Kwa mujibu wa mtandao
wa Telegraph, jana usiku ofisa wa shirika la kupambana na ugaidi Kenya
alikanusha taarifa kuwa Samantha Lewthwaite anaweza kuhusika na
shambulio la jana.

Samantha Lewthwaite aka The White Widow ni nani?
Ni mwanamke anayetafutwa kwa udi
na uvumba kwa kuhusika kwake kwenye matukio mbalimbali ya kigaidi
nchini Uingereza na Afrika Mashariki. Yeye ndiye aliyepanga shambulio
la kigaidi jijini London la mwaka 2005 lililosababisha vifo vya watu 52
ambapo mume wake Jermaine Lindsay alijitoa muhanga.

Akitokea Aylesbury,
Buckinghamshire, nchini Uingereza, The White Widow kwa sasa ni kiongozi
wa juu wa mashambulio ya Al Shabaab nchini Kenya na Somalia. Mwanamke
huyo anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa shughuli za kundi hilo la kigaidi.

Mwezi May hati ya kumkamata ilitolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani nchini Kenya kwa kesi ya kutengeneza bomu.

*anahisiwa* – Habari haijathibitishwa

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ