Top News

Tuesday, September 24, 2013

Rais KIKWETE amempa pole Uhuru kenyatta kwa shambulio lakigaidi.




Rais  Jakaya  Kikwete amezungumza kwa simu na rais Uhuru Kenyatta wa
Kenya na kumpa pole na kutaka kujua jinsi gani Tanzania inaweza kusaidia
kufuatia shambulio la kigaidi kwenye kituo cha biashara cha Westgate
katika eneo la Westlands, Nairobi, ambako watu 69 wameuawa na wengine
175 wamejeruhiwa. 

Rais Kikwete alimpigia simu rais Kenyatta  jioni ya Jumamosi

 kutokea mjini New York, marekani, mara baada ya kuwasili mjini humo

akitokea Toronto, canada, ambako alifanya ziara ya kikazi ya siku tatu.

Katika mazungumzo kati ya viongozi hao, rais Kikwete amemweleza rais

Kenyatta mshtuko na hasira yake kutokana na taarifa za kusikitisha za

shambulio hilo la kigaidi .

Katika salamu zake rais Kikwete amesema shambulio hili linalenga

kuitisha serikali na wananchi hodari wa Kenya na kudhoofisha nia yao ya

kutimiza wajibu wao wa kihistoria wa kuunga mkono jitihada za kuleta

amani katika nchi jirani na yenye matatizo ya Somalia. Rais amesema kwa

maana hiyo, shambulio hilo la woga na lisilo na huruma kabisa dhidi ya

watu wasiokuwa na hatia, lazima lilaaniwe na kushutumiwa vikali na

wapenda amani wote.

Amesema serikali na wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania

wanasimama bega kwa bega na kaka na dada zao wa Kenya katika kipindi

hiki kigumu. Aidha, serikali ya Tanzania inapenda kuihakikishia serikali

ya Kenya itaendelea kuiunga mkono na kushirikiana nayo katika kupambana

na balaa la ugaidi katika sura zake zote.

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ