Top News

Thursday, October 17, 2013

Hii ndio Video inayoonyesha Vizuri Wale Magaidi Waliovamia Westgate wakifanya yao bila wasi wasi

Kituo cha NTV cha Kenya kimeonesha video nyingine ya tukio la kuvamiwa kwa jengo la biashara Westgate jijini Nairobi mwezi uliopita inayoonesha vizuri zaidi magaidi wanne wakirandaranda ndani ya jengo hilo bila wasiwasi.

Katika video hii iliyochukuliwa na camera za CCTV za ndani ya jengo hilo, magaidi hao wanaonekana wakiwa wamebeba silaha nzito mikononi huku viunoni wamejifunga mikoba midogo. Wanaonekana wakijipanga ndani ya supermarket ya Nakumatt, mmoja wao alionekana akiwasiliana kwa simu huku wengine wakizunguka bila wasiwasi.
Sehemu ya video hiyo inaonesha magaidi wanne wakigawanyika katika makundi mawili na kushambulia kwa risasi mtu yeyote aliyejitokeza mbele yao.

Sehemu nyingine Katika video hiyo pia magaidi hao wanaonekana katika eneo moja la mlango mkubwa wa kutokea, hapo walionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa kiasi cha mmoja wao alionekana amekaa chini na mwingine aliweka silaha na kupiga magoti na kupiga dua.
Tazama video hapo juu

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ