Top News

Wednesday, October 16, 2013

Huu ndio Wimbo P square waliokanusha kuuimba ila unasauti kama zao, Aliyeuimba hajulikani.

Baada ya siku chache tangu wimbo mpya unaonekana kuwa wa kundi la P-Square kusambaa mtandaoni na mashabiki kuupenda, wasanii hao wamekanusha kuwa sio wimbo wao.

Wimbo huo ambao ni kweli una sauti kama zao, unaitwa Something About You. Pacha wa kundi hilo ambalo litakuja kutumbuiza nchini mwezi ujao, Peter Okoye amekuwa akiwaeleza mashabiki wengi wanaomuuliza kuhusu wimbo huo kuwa sio wao.
Swali ambalo wengi wanajiuliza ni nani aliyerekodi wimbo huo ulionza kupendwa?

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ