
Hii yote ni kuleta utofauti lakini wenye nguvu na utakaoleta shangwe zaidi kwa kila anaetia mguu Maishani ambapo kazi inapigwa na Dvj Majay kwenye mashine alafu Zungu Mnyama akawa anamiliki drums, kiufupi ni kwamba Zungu kazi yake kubwa ni kufatilizia nyimbo zinazopigwa na Majay kisha yeye anazigonga kwa ujuzi wa drums.
Unaweza kuchek video za hii style mpya Tanzania ambayo pia itaonyeshwa kwa wakazi wa Mtwara Jumamosi hii ya October 12 2013.


Kwenye hii video ya mwisho Snura ambae ni staa wa single za ‘Majanga’ na ‘nimevurugwa’ alionekana kwenye stage akionyesha ujuzi wake kwenye kukata viuno alafu mwishoni kwa bahati mbaya akaanguka wakati anataka kukinogesha..
Na Millard Ayo
No comments :
Post a Comment